27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

MESSI AMFUNGA BUFFON KWA MARA YA KWANZA

BARCELONA, HISPANIA

HATIMAYE mshambuliaji hatari wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi, amefanikiwa kumfunga mabao kwa mara ya kwanza mlinda mlango wa klabu ya Juventus na timu ya Taifa ya Italia, Gianluigi Buffon, kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya huku Barcelona ikishinda mabao 3-0.

Mchezo huo ambao ulipigwa juzi kwenye Uwanja wa Camp Nou, hatua ya makundi, Messi aliweza kuandika historia mpya ya kumfunga mlinda mlango huyo ambaye amekuwa akipata wakati mgumu kila anapokutana naye.

Messi alifunga bao lake la kwanza katika dakika ya 39 kipindi cha kwanza kabla ya kipindi cha pili kuongeza bao lake la pili huku lingine likiwekwa wavuni na Ivan Rakitic.

Buffon mwenye umri wa miaka 39, katika michezo mitatu ya Ligi ya Mabingwa waliyokutana na Barcelona, aliwahi kusema hawezi kufungwa na mchezaji huyo na atahakikisha anafanya hivyo kila wanapokutana, lakini juzi alishindwa kumzuia na kufanikiwa kuivunja historia hiyo.

Ilikuwa miaka 12 tangu Messi aanze kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya na kukutana na mlinda mlango huyo.

Kocha wa Juventus, Massimiliano Allegri, amedai alijua lazima apoteze mchezo huo kutokana na ubora wa wapinzani wao.

“Nawajua vizuri Barcelona, nadhani hii itakuwa mara ya 12 kukutana na timu hiyo, nimekuwa nikiujua uwezo wa Messi, siku zote ninawaambia wachezaji wangu kuwa mchezaji huyo ana uwezo tofauti lazima wawe makini.

“Bila ya kujali kuondoka kwa Neymar, lakini Barcelona bado ni klabu bora duniani kama ilivyo kwa Real Madrid, kukutana na timu hizo mara tatu bila ya kukufunga inakuwa jambo la historia.

“Ninaamini Barcelona na Real Madrid ni wababe wa Ligi ya Mabingwa, lakini kwa upande wetu naweza kusema huu ni mwanzo bado tuna nafasi ya kufanya vizuri,” alisema Allegri.

Mbali na mchezo huo wa Barcelona dhidi ya Juventus, mitanange mingine iliopigwa juzi ni pamoja na Chelsea ikishinda mabao 6-0 dhidi ya Qarabag FK, Sporting ikishinda mabao 3-2 dhidi ya Olympiacos, CSKA Moscow ikiichapa Benfica 2-1, AS Roma wakitoka bila kufungana dhidi ya Atletico Madrid na Man United ikishinda mabao 3-0 dhidi ya FC Basel, PSG wakishinda 5-0 dhidi ya Celtic na Bayern Munich wakishinda 3-0 dhidi ya Anderlecht.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles