27 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

MAYAY: SIMBA MKIMTIMUA OMOG MMEKWISHA

Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM

MCHAMBUZI maarufu wa soka nchini, Ally Mayay, amewatoa hofu mashabiki na wanachama wa Simba baada ya kusema anaamini kocha wao, Joseph Omog, atawapa mafanikio.

 

Simba ilizindua kampeni zake za Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu kwa ushindi mnono wa mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting kabla ya kutoka suluhu na Azam katika mchezo wa pili.

 

Suluhu hiyo iliwatia unyonge wapenzi wa Simba kutokana na kuamini timu yao ina kikosi imara ambacho kina uwezo wa kumtwanga mpinzani wao yeyote kutokana na kusajili wachezaji wenye ubora msimu huu.

 

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mayay ambaye ni kiungo wa zamani wa Yanga, alisema hana shaka na mfumo unaotumiwa na Omog, isipokuwa timu hiyo inahitaji muda wa kutosha wa kujijenga kabla ya kuwa na mwendelezo wa matokeo mazuri.

 

“Mfumo wa kutumia viungo wengi na mshambuliaji mmoja wa Simba si mpya, Omog ameukuta na hauna tatizo lolote, ni suala la kupewa muda ili ufanye kazi inavyotakiwa.

 

“Sioni tatizo lolote Simba kwa sasa maana wamefanya usajili wa wachezaji zaidi ya 10, kila mmoja ametoka katika timu iliyokuwa ikicheza mfumo tofauti, kwa hiyo subira inahitajika kabla ya kuwa na mashaka na uwezo wa kocha,” alisema Mayay.

 

Mayay alisema uongozi wa klabu hiyo utafanya kosa kubwa endapo utaamua kufanya mabadiliko katika benchi lao la ufundi.

 

“Utakuwa uamuzi wa hatari utakaoharibu kila kitu, timu imeanza msimu vizuri, ingawa wapo wanaokosoa mbinu za mwalimu Omog jambo ambalo nalipinga vikali.

 

“Hakuna jambo lolote zuri linalokuja kwa haraka, kama suala ni mfumo, Omog anajitahidi kuijenga Simba kulingana na uhalisia wa wachezaji alionao,” alisema Mayay.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles