27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 21, 2023

Contact us: [email protected]

Rotten Blood, Smaina watwaa tuzo ya Nyambago

CHRISTOPHER MSEKENA

KUNDI la muziki linalofanya vizuri Kanda ya Kati, Rotten Blood na Salim Kova ‘Smaina’, wameongoza orodha ya washindi waliotwaa tuzo za Nyambago zilizotolewa hivi karibuni jijini Dodoma mbele ya mgeni rasmi Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana, Antony Mavunde.

Akizungumza na MTANZANIA mwakilishi wakundi la Rotten Blood lililotwaa tuzo ya Kundi Bora la Mwaka, Myson Artist,alisema hiyo ni ishara kuwa muziki wao umekubalika ndani na nje ya Kanda yaKati na sasa hivi wana mpango wa kuendelea kutoa nyimbo kali ili kuwapa burudani mashabiki.

“Tunashukuru kwa kura nyingi ambazo mashabiki wametupigia hadi tumepata tuzo hii, kikubwa waendelee kutuunga mkono,”alisema Artist kutoka kundi la Rotten Blood linalotamba na wimbo wa Bata waliomshirikisha Linex.

Aidha, msanii Smaina kupitia wimbo Oliva alioshirikiana na Pam D na Mesen Selekta, alishinda tuzo ya Kolabo Bora ya Mwaka huku washindi wengine wakiwa ni Sonnatha Nduka (Mwigizaji Bora waKike), Danis David (Mwigizaji Bora wa Kiume), Davy Cobra (Chipukizi Bora),Banjalau (Msani Bora wa Hip hop) na Jacqueline Materu (Mtu mwenye Ushawishi).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles