26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Akon kinara kwa utajiri Afrika

LAGOS,NIGERIA

KWA mujibu wa Jarida la Forbes, staa wa muziki kutoka nchini Senegal, Aliaume Thiam maarufu kwa jina la Akon, ametajwa kuwa msanii anayeongoza kwa utajiri kwawasanii kutoka Afrika.

Jarida hilo limetoa majina 10 ya wasanii kutoka Bara la Afrika wenye utajiri mkubwa kwa mwaka 2018. Hata hivyo, Nigeria na Afrika Kusini wametoa idadi kubwa ya wasanii.

Akon ametajwa kuwa na utajiri wenye thamani ya Dola za Kimarekani 80, ambazo nizaidi ya Sh bilioni 183 za Kitanzania, huku akifuatiwa na Black Coffee kutoka nchini Afrika Kusini mwenye utajiri wenye thamani ya dola milioni 60, zaidi ya Shbilioni 137.

Wasanii wengine ni pamoja na Don Jazzy kutoka nchini Nigeria akiwa na dola milioni 30, zaidi ya bilioni 68. Wizkid anashika nafasi ya saba akiwa na kiasi cha dola milioni 20, zaidi ya bilioni 45, huku Davido akiwa na dola milioni 16 zaidi ya bilioni 36 na nafasi ya 10 ikishikwa na Oliver Mtukudzi.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,277FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles