Offset amkumbuka mama mtoto wake

0
1343

NEWYORK, MAREKANI

WIKI moja baada ya rapa, Offset kuachana na mama wa mtoto wake, Cardi B, rapa huyo ameweka wazi kukumbuka mapenzi yake.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Offset amedai tangu waachane, amekuwa akikosa furaha na amani kwa kuwa muda mwingi anatumia kumfikiria.

“Inaniumiza sana, kila wakati nakukumbuka Cardi B,” aliandika rapa huyo kutoka kundi la The Migos.

Taarifa ya kuachana kwao iliwekwa wazi na Cardi B kupitia ukurasa wake wa Instagram, ambapo aliweka wazi kuwa hawapo pamoja tena kwa kuwa hawakuzaliwa kwenye familia zenye upendo ndani yao.

Wawili hao waliweka wazi kufunga ndoa ya kimya kimya mwaka mmoja uliopita baada ya kuvujisha picha za ndoa yao, sasa wana mtoto mmoja mwenye umri wa miezi sita.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here