22.3 C
Dar es Salaam
Saturday, July 13, 2024

Contact us: [email protected]

Rose Mhando ndani ya Tamasha la Pasaka

Rose mhandoNA MWANDISHI WETU

MWIMBAJI nguli wa muziki wa injili Afrika Mashariki, Rose Mhando, amekuwa wa pili kuthibitisha kushiriki katika Tamasha la Pasaka linalotarajia kufanyika mikoa ya Geita, Mwanza na Wilaya ya Kahama.

Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama, alisema Rose ameungana na mwenzake, Bonny Mwaitege katika tamasha hilo la mwaka huu linalotarajiwa kufanyika Geita (Machi 26), Mwanza (Machi 27) na Kahama (Machi 28).

Aidha, Msama alisema dhamira ya Tamasha la Pasaka ni wenye uhitaji maalumu ambao ni yatima, walemavu na wajane.

Msama alisema sababu ya kupeleka Tamasha la Pasaka mikoa ya Kanda ya Ziwa ni kufikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa wakazi wa mikoa hiyo sambamba na kupiga vita mauaji ya walemavu wa ngozi ‘albino’.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles