24.6 C
Dar es Salaam
Thursday, September 28, 2023

Contact us: [email protected]

Video za Beyonce, Rihanna zawa kivutio mitandaoni

rihanna-drake-workNEWYORK, MAREKANI

WAKATI Beyonce akitambulisha video ya wimbo wake mpya wa ‘Formation’ aliomshirikisha Blue Ivy, mrembo mwingine katika muziki nchini Marekani, Rihanna naye ameachia baadhi ya vipande vya video ya wimbo wake mpya wa ‘Work’ alioshirikiana na Drake.

Beyonce akiwa ameutambulisha wimbo huo unaoonekana kumtambulisha upya katika ramani ya muziki wake huku Rihanna naye akaachia baadhi ya vipande vinavyoonyesha video yake itakavyokuwa jambo ambalo limewapa hamu kubwa mashabiki wake kutaka kuiona video hiyo ikitoka haraka.

Vipande vya wimbo wa Rihanna na Drake vinawaonyesha wakiwa katika mjumuiko wakifurahia pamoja huku kila mwenye kinywaji na asiye na kinywaji akicheza ama kufurahia kinachoonyeshwa na wanenguaji waliojaa eneo hilo.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,745FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles