27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

RONALDO, ZIDANE MUNGU AMEWAUMBA NA BAHATI ZAO

BADI MCHOMOLO NA MITANDAO


HAKUNA kinachoshindikana chini ya jua, ndiyo kauli ambayo ipo duniani, ikiwapa watu matumaini ya kufanya mambo magumu kuwa rahisi.

Wengi tulikuwa tunaamini kuwa haiwezekani Kombe la Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kuchukuliwa mara mbili mfululizo na klabu yoyote, kumbe si kweli, kauli hiyo ya upotoshaji imevunjwa na Real Madrid usiku wa kuamkia jana.

Hakuna kisichowezekana chini ya jua, Real Madrid wamefanikiwa kutwaa taji hilo kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuichapa Juventus mabao 4-1, katika fainali iliyopigwa mjini Cardiff.

Tulilazimishwa kuamini kuwa haiwezekani Madrid kuchukua taji hilo mara mbili, lakini Madrid wametulazimisha tuamini kuwa hakuna kitu kisichowezekana duniani.

Historia imeandikwa kwa miamba miwili ya soka ndani ya kikosi hicho, ambao ni Cristiano Ronaldo ambaye aliongoza safu ya ushambuliaji na kocha wa timu hiyo, Zinedine Zidane.

Ronaldo aliiweka historia mpya ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao katika fainali tatu za Ligi ya Mabingwa alizocheza, lakini pia katika mchezo huo wa juzi alikuwa mwiba kwa wapinzani wake, huku akifunga mabao mawili peke yake.

Katika michuano hiyo amekuwa kinara wa ufungaji bora, akiwa na mabao 12, huku mpinzani wake wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi, akiwa na mabao 11.

Si Ronaldo pekee ambaye amekuwa na bahati katika kikosi hicho, ni karibu wachezaji wote ambao walikuwa kwenye kikosi hicho msimu uliopita na kutwaa taji hilo na mwaka huu wakiwamo tena.

Ronaldo ameibuka mfungaji bora kwenye michuano hiyo, pia alikuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha timu hiyo inatwaa Ligi Kuu nchini Hispania msimu huu, kuna uwezekano mkubwa akatwaa tuzo ya Ballon d’Or msimu huu kutokana na mafanikio makubwa. Ni bahati ya kipekee.

Zidane ni miongoni mwa watu ambao wamepewa bahati na Mungu, huku ikiwa ni siku 512 tangu apewe kibarua cha kuwa kocha mkuu Januari 9, 2016 hadi Juni 3, 2017 na sasa amefanikiwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa mara mbili, Ligi Kuu mara moja msimu huu, Uefa Super Cup mara moja na Kombe la dunia la klabu.

Hakuna ambaye aliamini kuwa angeweza kuvaa vizuri kiatu cha Rafael Benitez, ambaye alichukua nafasi yake baada ya kufukuzwa kazi kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo.

Rais wa timu hiyo, Florentino Perez, alikuwa kama anajaribu kumpa Zidane timu hiyo, ikiwa ni kibarua chake cha kwanza kwa timu kubwa tangu awe kocha, lakini aliyoyafanya kwa siku 512 yametosha kumshawishi Perez aseme kuwa Zidane atakaa ndani ya kikosi hicho hadi mwisho wa maisha yake.

Wakati anapewa timu hiyo na kutwaa Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza, Perez alimwambia lengo la timu hiyo si Ligi ya Mabingwa, ni Ligi Kuu, hivyo kama utashindwa kulipata basi unatakiwa kuondoka, lakini alichokifanya Zidane ni kuchukua mataji yote muhimu na kumfunga mdomo Perez.

Hata hivyo, Zidane ameonekana kuwakosea sana Juventus kwa kuchukua ubingwa, wakati huo mwaka 1996 anajiunga na Juventus na kucheza jumla ya michezo 151 ya Ligi Kuu hadi mwaka 2001 alishindwa kutwaa taji hilo, mbali na kushiriki kwenye michuano, lakini leo hii akiwa kocha ndani ya Madrid anachukua mara mbili mfululizo. Mungu amewaumba watu na bahati zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles