23.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 22, 2023

Contact us: [email protected]

Ronaldo aweka rekodi ya mabao 700

KIEV, UKRAINE

MCHEZAJI bora duniani, Cristiano Ronaldo, juzi aliandika historia mpya ya kufikisha jumla ya mabao 700 aliyoyafunga katika maisha yake ya soka la kulipwa.

Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa Ureno, alifunga bao moja kwenye mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya Euro 2020, lakini Ureno ilikubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Ukraine.

Ronaldo ambaye anakipiga katika klabu ya Juventus, alisema kitendo cha kuweka rekodi mbalimbali kinakuja chenyewe. Bao hilo la 700 alilifunga kwa mkwaju wa penalti kipindi cha pili cha mchezo huo.

Hata hivyo Ureno ilikubali kichapo hicho ambacho ni chakwanza kukipata tangu kumalizika kwa michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi mwakani jana.

“Kufikisha idadi hii ya mabao sio kama kila mchezaji anaweza kufanya, lakini nitumie nafasi hii kuwashukuru wachezaji wenzangu, makocha kwa kunifanya niwe mchezaji kama nilivyo sasa. Mbali na kufurahia rekodi hii, lakini nimechukizwa kwa kitendo cha kushindwa kupata ushindi dhidi ya wapinzani,” alisema mchezaji huyo.

Hata hivyo alipoulizwa juu ya mafanikio yake mwenyewe, Ronaldo alisema, “Kwani nina rekodi ngapi hadi sasa? Sijui, lakini natakiwa kufurahia hali hii na kuwashukuru wale wote ambao wamenifanya niwe hapa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles