27.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

RIPOTI YA CAG YAZIDI KUANIKA MADUDU


Na FREDY AZZAH-Dodoma   |    

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad, amewasilisha bungeni ripoti yake ya ukaguzi kwa mwaka unaoishia Juni 2017, ambayo imeibua madudu zaidi na kuonyesha deni la taifa likiwa limefikia Sh trilioni 50.

Akitoa muhtasari wa ripoti yake kwa waandishi wa habari mjini hapa jana, alisema ukaguzi wake umejikita kwenye maeneo sita.

Aliyataja maeneo hayo ni ukaguzi katika Serikali kuu, mamlaka za Serikali za mitaa, mashirika ya umma, miradi ya maendeleo, ukaguzi wa ufanisi na ripoti 10 za ukaguzi wa ufanisi kwenye sekta mbalimbali.

Ripoti hiyo ya CAG imeonyesha uozo pia kwenye mafuta yaliyosamehwa kodi, udhibiti mizigo inayosafirishwa nje ya nchi, urejeshwaji mikopo, udhaifu katika usimamizi wa mikataba ya manunuzi, mapato kutowasilishwa kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali na mawakala kutowasilisha makusanyo kwenye mamlaka za Serikali za mitaa.

Uozo mwingine umeibuliwa kwenye Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Shirikisho la Serikali za Mitaa (ALAT) na Idara ya Uhamiaji.

Akizungumzia deni la taifa, Profesa Assad alisema limefikia Sh trilioni 50 na kwamba ni vyema kama nchi ikakopa kwa tahadhari ili isirudi nyuma miaka 20 ambako ilisamehewa sehemu ya deni.

Alisema hadi kufikia Juni 30, 2017, deni hilo lilikuwa Sh trilioni 46.08 kutoka Sh trilioni 41.03 za Juni 2016, ikiwa ni ongezeko la Sh trilioni 5.04 sawa na asilimia 12.

Profesa Assad alisema deni la ndani ni Sh trilioni 13.33 na deni la nje ni Sh trilioni 32.75.

Alisema katika deni hilo, kuna Sh trilioni 4.58 ambazo hazikujumuishwa kutokana na ….

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles