24.6 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

JPM: KIKWETE AMEIMARISHA DEMOKRASIA


Na NORA DAMIAN-DAR ES SALAAM    |

RAIS Dk. John Magufuli amemmwagia sifa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete kwa kuliongoza taifa vizuri, akisema aliimarisha demokrasia nchini wakati wa utawala wake.

Alisema Rais Kikwete alilitumikia taifa la Tanzania kwa uadilifu na uaminifu mkubwa, hasa wakati akiwa rais.

Akizungumza jana wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Jakaya Kikwete (JMKF) uliofanyika Ikulu, alisema Kikwete alisimamia ukuzaji wa demokrasia na kuitangaza vema nchi, alisimamia mageuzi ya kiuchumi na ujenzi wa miundombinu.

“Sisi wanadamu hatuna kawaida ya kuwasifu watu wakiwa hai, akifa mtu tunasema pengo lake halizibiki, leo (jana) mimi naomba nikusifu mzee Kikwete ukiwa hapa nakuangalia na kutabasamu, hongera sana.

“Mzee Kikwete alisimamia vizuri mageuzi ya kiuchumi, afya, miundombinu, elimu, maji, ukuzaji wa demokrasia na alitangaza nchi yetu kimataifa.

“Mheshimiwa Rais mstaafu tunakukumbuka, kwa hakika umefanya mambo mengi sana na nina hakika mchango wako utaendelea kukumbukwa vizazi na vizazi. Watanzania watake au wasitake, wataendelea kukukumbuka.

“Alisimamia ujenzi wa shule za kata, Chuo Kikuu cha Dodoma, Hospitali ya Mloganzila, hata bomba la gesi la kutoka Kusini hadi Dar es Salaam umelifanya wewe (Kikwete),” alisema Rais Magufuli.

Alisema mbali ya Kikwete kuwa rais wa nchi, alishika nyadhifa mbalimbali ndani na nje ya nchi kama vile Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), mjumbe wa jopo la watu mashuhuri la kumshauri Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu lishe, afya ya wanawake, watoto na vijana, balozi wa heshima wa chanjo duniani na sasa ni mwakilishi wa AU kwenye mgogoro wa Libya.

“Kwa kuzingatia hayo yote, ameona aendelee kuitumikia nchi yetu na Bara la Afrika kupitia taasisi aliyoianzisha. Nakupongeza sana, kwa hakika umefanya jambo jema.

“Kustaafu si mwisho wa kutoa mchango wako kwa taifa, kustaafu ni hatua tu, umeiga mifano ya Mwalimu Nyerere na Mkapa, na hii inapaswa kuwa changamoto kwa wastaafu na wazee wengine,” alisema.

 

ALIMBEBA URAIS

Rais Magufuli alisema ataendelea kumshukuru Kikwete kwani bila yeye huenda asingekuwa rais …

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya MTANZANIA.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles