RIPOTI YA AJALI YA NDEGE YA ETHIOPIA KUTOLEWA WIKI HII

Serikali ya Ethiopia imesema ripoti ya awali kuhusu ajali ya ndege ya Boeing 737 Max 8, ambamo watu 157 waliuawa huenda ikatolewa wiki hii.

Haikutoa maelezo zaidi juu ya tarehe ya uhakika kutolewa ripoti hiyo, wala dondoo kuhusu ugunduzi wake.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Nebiat Getachew, amesema Wizara ya Usafirishaji itatoa ripoti ya awali juu ya uchunguzi wake wa ajali hiyo iliyotokea Machi 10, ambamo ndege hiyo ya Boeing 737 Max 8 ilianguka muda mfupi tu baada ya kuruka kutoka Addis Ababa.

Wizara ya Usafirishaji ambayo ndiyo inahusika na uchunguzi huo, ilisema baadae kuwa bado itachukuwa siku kadhaa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here