30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

NMB benki inayoongoza kutoa hisani kwa jamii

Shermarx Ngahemera

BENKI ya NMB kupitia dhima yake ya kurudisha sehemu ya faida inayopata kwa jamii inafanya wajibu huo kwa ufanisi mkubwa bila hiyana na kwa mwaka huu ameweka kipaumbele kwenye miradi ya elimu na afya kwa jamii mbalimbali nchini na kuwa kinara wa utoaji michango hiyo.

Kwa mwaka huu hadi wiki iliyopita Benki hiyo imeshatoa kiasi cha zaidi ya shilingi  Milioni 400/- na nyingine nyingi ziko njiani kutolewa kwa wafaidika mbalimbali kuzingatia utayari wa wahusika na utatuzi wa mambo husika kwa kadiri yalivyoombewa na eneo la CSR kuanzia  mwezi Januari hadi sasa ili kusaidia miradi ya maendeleo ya jamii katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Sisi  tunachombeza tu kwenye mambo makubwa ambayo serikali inafanya kwenye elimu na afya ikiwamo ujenzi wa zahanati 700 na vituo vya afya  kila kijiji, shule za sekondari na  mabweni ya shule  za wasichana  na madarasa yakiwamo maabara zake. 


Filbert Mponzi  ni Mkuu Biashara ya Benki na Serikali anasema  serikali ina stahili kupongezwa na kuungwa mkono kwa yale mazuri inayofanya kama inavyoaminika kuwa mcheza kwao hutunzwa.

Mponzi anasema Serikali inafanya makubwa katika sekta za afya na elimu ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma za matibabu na elimu, katika maeneo ya mijini na vijijini. NMB,  alisema Mponzi kama mtoa huduma wa kifedha, alisema kuwa wanapenda sana kusaidia jamii, zinazowazunguka kwa kuwapa sehemu ya faida yao.  Ili zilete mabadiliko chanya kwa  wafaidika wake.


Alisema kuwa katika kipindi cha mwezi huu, wametoa zaidi ya milioni  65m / – kwenda shule, hospitali na vituo vya afya katika maeneo mbalimbali ya nchi.
“Kwa mfano, tuliwapatia madawati yenye thamani ya shilingi milioni 5 / – kwa Sekondari ya Buswelu katika Wilaya ya Ilemela, tuliwapa vifaa vya thamani ya shilingi milioni 10/ – Shule ya sekondari Kakola  na Kituo cha Afya cha Karumwa katika Wilaya ya Nyang’hwale, vifaa vya kuezekea paa vilivyofikia shilingi milioni  10 / – kwa Shule ya Msingi ya Lugala. Wilaya ya Morogoro, “aliongeza.


Alisema misada iliyotolewa ni mingi  ikiwamo pamoja na   shilingi milioni 5 / – Mkoa wa Kigoma, misaada mengine katika orodha ni  shilingi milioni 5 / – kwa Chalinze, na shilingi milioni  5 / – kwa Hospitali ya  Kaliua kwa vifaa vyao vya ndani. “Wakati Hospitali ya Butimba katika Wilaya ya Nyamagana ilipokea vifaa vya thamani ya milioni 10 / – Jumatatu tarehe 25 mwezi huu,” alisema Mponzi.

Eveta Ngawaia ni mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mulua katika Wilaya ya Kondoa, alisema kwa upande wake, msada wa benki hiyo umewapa uwezo wa kununua madawati mengine, ambayo yatasaidia kutoa viti kwa wanafunzi wao waliokuwa wakiketi  chini.


Kwa Hospitali ya Kaliua, Mganga  Mkuu Dk Aristides Raphael, alifurahia mchango wa benki wa vitanda kwa wodi namba 5 na kitanda cha kujifungulia na shuka 54 zitapunguza  uhaba wa vifaa hospitalini hapo.

Ukitazama kiwango cha misaada inayotolewa unaweza kusema ni kidogo lakini kihali ni mwafaka na inatolewa ili kufaa watu wengi na taasisi nyingi kimkakati kwani mahitaji ni makubwa zaidi. Uongozi wa NMB unasisitiza kuendele kutoa misaada kulingana na bajeti na mapato yake ila kiujumla wamepanga kutoa asilimia moja ya faida yake kwa mwaka husika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles