26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 27, 2021

RICO SINGLE: ZANZIBAR NGUMU KUIMBA KAMA NEY

Na MWANDISHI WETU, ZANZIBAR


MWANAMUZIKI wa muziki wa Bongo Fleva anayefanyia shughuli zake za muziki visiwani Zanzibar, Rico Single, ameweka wazi kwamba, kuimba wimbo wa harakati kama alivyofanya Emmanuel Elibarik (Nay wa Mitego) ni vigumu kwa Zanzibar, kwa madai kwamba mitazamo ni tofauti.

Rico Single alisema siasa visiwani humo ina nafasi kubwa mno na kama msanii atajaribu kuimba wimbo kama huo, huenda akakutana na matatizo makubwa kutoka kwa mtu mmoja mmoja hata kama si mlengwa aliyeimbiwa wimbo huo.

“Huku bana watu wanapenda siasa kuliko fedha, ukiimba harakati kama za wimbo wa Ney utajikuta katika matatizo, maana mtu tu mwenye mapenzi na unayemuimba anaweza kukudhuru kabla hata mlengwa mwenyewe hajakufikia, ndiyo maana harakati huku zimepungua kwa wasanii,’’ alieleza Rico Single.

Rico Single aliongeza kwamba, baadhi ya wasanii wa bongo fleva walishawahi kuimba nyimbo zenye ujumbe wa harakati kwa kuikumbusha serikali mambo maovu yanayofanywa na watu visiwani humo, lakini mapokeo yake yakawa tofauti.  

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,388FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles