RENARD ACHIMBA MKWARA AFCON

0
636

LIBREVILLE, GABON


FOOTBALL : Sochaux vs Monaco - Ligue 1 - 20/10/2013KOCHA aliyetamba kwa miaka ya hivi karibuni katika michuano ya Mataifa ya Afrika ‘Afcon’ Herve Renard, amechimba mikwara ya kutwaa taji hilo ambalo linatarajia kuanza kutimua vumbi kesho nchini Gabon.

Kocha huyo amedai kuwa atahakikisha anafanikisha kutwaa ubingwa wa michuano hiyo msimu huu ili iwe mara yake ya tatu kulitwaa taji hilo.

Renard raia wa nchini Ufaransa ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha Morocco, wengi wanaamini kuwa kocha huyo hawezi kufanya lolote msimu huu katika michuano hiyo kutokana na wachezaji wake wengi nyota kuwa majeruhi.

Hata hivyo, kocha huyo amedai kuwa hana wasiwasi na baadhi ya wachezaji wake kuwa majeruhi, atahakikisha anapambana ili kutwaa taji hilo kama ilivyo wakati anaifundisha timu ya Ivory Coast miaka miwili iliyopita na kutwaa taji hilo.

“Nitahakikisha natwaa kombe hili kwa urahisi zaidi nikiwa na timu hii, nakumbuka wakati naifundisha Ivory Coast na kutwaa ubingwa wengi hawakuamini kama ningeweza kufanya hivyo kwa kuwa nilikuwa na kikosi ambacho kilikuwa kinasua sua.

“Kwa upande wangu ninaamini hakuna kinachoshindikana katika soka, hivyo lengo langu ni kutwaa ubingwa wa michuano hii kwa mara ya tatu,” alisema Renard.

Kocha huyo awali alifanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano akiwa na kikosi cha timu ya taifa ya Zambia mwaka 2012 pamoja na Ivory Coast mwaka 2015 na sasa anatarajia kutwaa akiwa na kikosi hicho cha Morocco.

Hadi sasa ni makocha wawili tu ambao wamefanikiwa kutwaa taji hilo mara tatu ambao ni Charles Gyamfi ambaye alitwaa akiwa na timu ya Ghana mwaka 1963, 1965 na 1982, huku Hassan Shehata, akitwaa akiwa na Misri mwaka 2006, 2008 na 2010.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here