ONYANGO FITI KUIVAA GHANA

LIBREVILLE, GABON


Onyango1UONGOZI wa timu ya taifa ya Uganda ‘The Cranes’, umeweka wazi kuwa mlinda mlango wao namba moja, Denis Onyango, atakuwa fiti kupambana katika mchezo wa kwanza wa ufunguzi dhidi ya Ghana kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.

Mchezo huo wa kwanza kwa timu hizo utapigwa Januari 17 kwenye uwanja wa Stade de Port Gentil, ambapo uongozi wa timu hiyo ya Uganda ulikuwa na wasiwasi baada ya kipa huyo kuumia katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Ivory Coast juzi.

Kipa huyo wa klabu ya Mamelodi Sundowns, aliumia nyonga katika dakika ya 38 ya mchezo huo wa kirafiki ambapo Uganda ilikubali kichapo cha mabao 3-0, lakini kutokana na matibabu aliyoyapata madaktari wa timu wamethibitisha atakuwa vizuri katika mchezo wao wa kwanza.

“Nina imani kwamba nitakuwa sawa katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya Ghana, naendelea vizuri na matibabu hivyo mashabiki wa timu hii wasiwe na wasiwasi na hali yangu,” alisema Onyango.

Madaktari wa timu hiyo, Ronald Kisolo na Ivan Ssewanyana, wamepewa jukumu la kumwangalia mchezaji huyo kwa hali ya juu ili kuhakikisha anacheza katika mchezo wa kwanza ambao kwao wanaamini kuwa ni mgumu.

Uganda wanataka kuingia uwanjani huku wakiwa na lengo la kutaka kulipa kisasi cha mwaka 1978 ambapo Uganda walipokea kichapo cha mabao 2-0 katika hatua ya fainali ambayo ilipigwa nchini Ghana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here