26.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, January 18, 2022

RC: MARUFUKU KUUZA MAHINDI SHAMBANI

Na ELIUD NGONDO-SONGWE


MKUU wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa, amewazuia wafanyabiashara wa zao la mahindi mabichi wanaonunua kwa wakulima kupitia njia za wizi mkoani humo, waache mara moja kabla sheria haijachukua mkondo wake.

Mkuu huyo wa mkoa aliyasema hayo jana wilayani Ileje wakati wa sherehe za Mei Mosi zilizofanyika juzi na kusisitiza kuwa msako mkali utaanza wiki ijayo.

Alisema amepiga marufuku wananchi kuuza mahindi kwa wafanyabiashara kutokana na wengi wao kuwadanganya wakulima.

Alisema kuna baadhi ya wafanyabiashara wameingia mkoani humo kinyemela na kuanza kuwarubuni wananchi kuanza kuuza mahindi mabichi ambayo hayajakauka.

Alisema licha ya mkoa huo kuonekana una mahindi ya kutosha, kuna hatari kubwa ya kuwa na uhaba wa chakula baadaye kama wafanyabiashara hao wataachwa waendelee kununua.

“Kuna baadhi ya wafanyabiashara kutoka maeneo mbalimbali katika mkoa wetu, wanawashawishi

wananchi kuuza mahindi mabichi yanayotoka shambani, kuanzia sasa waondoke na wananchi hawaruhusiwi

tena kufanya biashara hii.

“Tunaweza tukajisifu kuwa tumezalisha chakula cha kutosha, tukiwaacha hawa watu wakaendelea na biashara hii, tutajikuta baadaye tunaingia kwenye janga, watendaji wote wa Serikali tunatakiwa kusimamia hili agizo,” alisema.

Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Joseph Mkude, aliwataka watumishi wote wa Serikali wilayani humo kuwa walinzi katika maeneo yao kwa kuhakikisha katazo hilo linazingatiwa.

Alisema hata baada ya mahindi yote kuvunwa shambani, mwananchi hawezi kuuza kwa mfanyabiashara yeyote atakayetaka kununua, lazima akachukuwe kibali kwa mkurugenzi wa wilaya.

Alisema kuanzia sasa mipaka yote ya kutoka na kuingia katika wilaya hiyo itadhibitiwa ili kuzuia wafanyabiashara hao.

Baadhi ya wananchi walisema wameanza kuuza mahindi hayo kutokana na kipato chao kuwa kidogo.

Mkazi wa Ileje, Isaya Nzunda, alisema wakulima wamekuwa wakikosa mahitaji mengine kutokana na ukosefu wa fedha.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
174,922FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles