25.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

RC MAKONDA AMPELEKA INDIA MSHINDI WA BSS KWA MATIBABU

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda ametimiza ahadi ya kusaidia gharama za matibabu ya mshindi wa BONFO Star Search (BSS) 2009, Pascal Cassian kwa kufanikisha kumpeleka nchini India kwa matibabu.

Mkuu huyo wa mkoa amemkabidhi tiketi ya ndege, pesa ya nauli, chakula, hotel na ya kujikimu kwa watu watatu watakaomsindikiza akiwemo mke wake na mkuu wa kitengo cha Urolojia Hospital ya Taifa Muhimbili watakaoambatana naye.

RC Makonda amesema uamuzi wa kumpeleka nchini India umekuja baada ya Jopo la madaktari bingwa wa Muhimbili kuridhia kwamba msanii huyo apelekwe Hospital ya kimataifa huko India kwa matibabu zaidi ya tatizo hilo.

Aidha RC Makonda amewashukuru watanzania wote waliochangia na kufanikisha safari hiyo huku akiwaomba waendelee kuwa na moyo huohuo wa kusaidiana kwenye matatizo.

Naye Pascal amemshukuru RC Makonda kwa kumsaidia kwani anaamini Mungu atamsaidia atarejea nchini akiwa amepona na kurudi katika afya yake ya kawaida.

Awali RC Makonda alimsaidi Pascal kwa kumtoa nyumbani kwake na kumpeleka hospital baada ya kuona akiomba msaada wa matibabu kupitia kwenye mitandao ya kijamii baada ya kupata ajali iliyopelekea tatizo kubwa la kwenye mfumo wa figo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,784FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles