23.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 22, 2023

Contact us: [email protected]

RC azipa h’shauri siku tano kuhamisha fedha

NA AMON MTEGA-RUVUMA

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma,  Christina Mndeme ametoa siku tano kwa halmashauri za wilaya kuhakikisha fedha  za miradi  ya maji zilizokuwa kwenye akaunti zao kuhamishiwa  kwenye akaunti ya za Wakala wa Usambazaji  wa Maji Safi na Mazingira Vijijini (Ruwasa) ili mamlaka hiyo iweze kukamilisha miradi kwa wakati.

Agizo hilo alilitoa  jana wakati  akisimamia makubaliano na kukabidhiana mikataba baina ya halmashauri na RUWASA mjini Songea.

Alisema fedha zinazotakiwa zihamishiwe kwenye akaunti ya wakala huo, ni zaidi ya Sh  bilioni moja ambazo zitatumika kakamilisha miradi mikubwa ya maji.

Alisema baadhi ya miradi hiyo, imekuwa ikisuasua kutokana na kutokusimamiwa kikamilifu kwa wakandarasi waliopewa kazi.

Alisema hadi kesho fedha hizo ziwe zimeshahamishwa na siyo vinginevyo  na kuwa miradi hiyo itakamilika kwa kutumia mfumo wa fosi akaunti.

Alisema Rais Dk. John Magufuli ameunda chombo hicho ili kufanikisha kusambaza maji kwa wananchi kwa wakati.

Alisema miradi hiyo, itafanyiwa kazi na wakala wenyewe kwa kushirikiana na wananchi hadi ifikapo mwaka 2020 huduma hiyo iwe imewafikia asilimia 85 au zaidi na kufanya kila maeneo ya vijiji na mijini kutokuwa na tatizo la maji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles