23.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 22, 2023

Contact us: [email protected]

CCM wagoma kupiga kura za maoni

NA Elizabeth Kilindi,Njombe.

WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kijiji cha Igwachanya, wamegoma kupiga kura za maoni za kumchagua mwakilishi ambaye atagombea nafasi ya mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho.

Hatua hiyo, imekuwa  baada ya jina la mgombea mmoja ambaye ni mwenyekiti anayemaliza muda wake kutotajwa tena, licha ya kuchukua fomu ya kutetea nafasi yake.

Wakizungumza na MTANZANIA baada ya kugomea uchaguzi  wa ndani ya chama hicho juzi, wanachama  hao walisema  hawawezi kumchagua mtu yeyote kwa madai uchaguzi si halali.

“Uchaguzi huu, ni wa kihuni mwenyekiti wa awali wamemtoa, tunakiongozi ambaye alikuwapo ndiyo maana tumegomea hatuwezi kufanya uchaguzi huo,’’alisema Dickson Kiswaga.

Naye Tito John,  alisema”Kuna mgombea tumekuja kuchagua ila kwa sababu ya wizi wa viongozi wa CCM kijiji kutaka kututeulia viongozi wanaowataka wao, tumesikia fununu wanakutana kuzungumza eti wanamtaka mtu mwingine ili kusudiaje awasaidie kwenye uchaguzi mkuu’’.

‘’Mimi nimegomea kwa sababu jina la kiongozi wangu sijaliona,hatujatendewa haki kama chama chenyewe kinafanya ufisadi,kama walimpendekeza mtu wanaomjua wao wasingetuita,’’alisema Lazaro Kilamlya.

Akisoma majina ya wagombea ambao wamepewa nafsi ya kuwania nafasi hiyo,Msimamizi wa Uchaguzi,Vumilia  Kilamlya alitaja majina matatu huku jina la nne ambalo ni la mwenyekiti ambaye yupo madarakani kwa sasa halijatajwa.

Kwa upande wa mgombea  ndani ya chama hicho, akiwamo Laulence Ngilangwa alisema wameshangazwa na kitendo cha wanachama kugomea uchaguzi huo na kuwataka kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kwa kuwa watampata kiongozi ambaye wanamtaka.

Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho, Jafari Kaganga ambaye amegombea kwa mara nyingine tena nafasi hiyo alisema anashangazwa na kitendo cha jina lake kukatwa kwa kuwa amekuwa akisimamia shughuli za kimaendeleo ipasavyo.

Katibu wa CCM Wilayani ya  Wanging’ombe, Juma Nambaila alisema chama kina taratibu zake za kumpata mgombea anayefaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles