25.7 C
Dar es Salaam
Saturday, December 4, 2021

RAY C AWACHANA WAPENDA KIKI

 

 

NA JESSCA NANGAWE

MKONGWE wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila (Ray C) amesema ipo haja ya wasanii kuacha kutumia kiki, kwa kuwa ubora wa kazi zao unajiuza wenyewe.

Ray C, ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake ya Unanimaliza, amesema anazidi kujipanga ili kuwadhihirishia mashabiki zake kuwa kwa sasa anaheshimu kipaji chake na amerudi kwa miguu yote kwenye muziki.

“Kama mashabiki wanataka muziki mzuri watapata, kama wanataka muziki wa kiki si rahisi, kwa kuwa muziki wa sasa unaendeshwa kisasa zaidi na hakuna maigizo. Siwezi kufanya muziki wa kiki kwa sababu mimi ni msanii halisi, sibebwi, kama nimeweza kupita kipindi kile ina maana nina kipaji halisi,” alisema Ray C.

Aliongeza kuwa, wapo wasanii wanaofanya vizuri bila kutegemea kiki na kazi zao zimekuwa zikikubalika sana, hivyo ni wakati wa kubadilika na kuendana na kasi ya teknolojia ya sasa.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,897FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles