26.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 26, 2023

Contact us: [email protected]

RAYVANNY: NYIMBO ZANGU HAZITACHUJA

 

 

 

NA JESSCA NANGAWE

MSANII kutoka lebo ya WCB, Raymond, maarufu kama Rayvanny, amesema pamoja na kutoa nyimbo mfululizo, haamini kama zitachuja mapema, kwa kuwa anafanya kazi zake kwa malengo.

Maneno ya Rayvanny yanakuja siku mbili baada ya kuachia video ya ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Chuma Ulete’, huku akiahidi kuendelea kutoa nyimbo mfululizo.

Alisema wasanii wengi wamekuwa wakiogopa kutoa nyimbo mfululizo kwa hofu ya kuchuja mapema, lakini amesisitiza hakuna ukweli wowote, kikubwa ni kuhakikisha msanii anakuwa mbunifu.

“Unajua wasanii wengi tumekuwa waoga kwa kuwa hatuna ubunifu wa kutosha na ndiyo maana hata mara nyingi msanii anadiriki kusema hawezi kutoa nyimbo mfululizo kwa kuwa anaogopa atachokwa na mashabiki, tubadilike na kuendana na matakwa ya mashabiki zetu,” alisema Rayvanny.

Aliongeza kuwa, baada ya kuachia ngoma hiyo, amepanga kutoa nyingine mfululizo kwa kuwa anaamini zina ubora na haziwezi kupoteza mvuto kwa mashabiki zake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,726FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles