25.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

RAIS XI JINPING AILILIA NEW ZEALAND KUHUSU HUWAWEI

Rais wa China Xi Jinping ameitaka New Zealand kutobagua makampuni ya China wakati alipokutana na Waziri Mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern, ambaye nchi yake ilikataa ombi la kampuni la China la masuala ya mawasiliano Huawei kujenga mtandao wa simu za mkononi wa 5G.

Ardern, akiwa katika ziara ya siku moja nchini China, alisema kabla ya mkutano na Xi kwamba ana matumaini ya kuwa na majadiliano na Serikali ya China juu ya uamuzi wa shirika la New Zealand la intelijensia kukataa ombi hilo.

Mahusiano na China yameingia katika hali ya wasi wasi chini ya serikali ya Ardern ambayo imeonesha wazi wasi wasi wake juu ya kuongezeka kwa ushawishi wa China katika eneo la kusini mwa bahari ya Pasifiki.

Wakikutana mjini Beijing Xi alimwambia Ardern kwamba China imekuwa wakati wote ikiiangalia New Zealand kama rafiki na mshirika mwaminifu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,784FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles