23.6 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

NINA MATUMAINI YA MUSTAKABALI WA LIBYA:GUTERRES

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ana matumaini kwa ajili ya suluhu ya mgogoro wa miaka minane wa Libya baada ya kushiriki mkutano wa ngazi ya juu leo Jumamosi mjini Tunis Tunisia.

Mkutano huo wa Jumuiya ya nchi za Kiarabu au Arab League umejumuisha maafisa kutoa nchi za Kiarabu, Muungano wa Ulaya na Muungano wa Afrika.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Katibu Mkuu amesema “ Baada ya kuwa na mkutano wenye ufanisi na washirika wetu kuhusu Libya Quartet, neno ambalo linaelezea ninachohisi kuhusu Libya hivi leo ni tumaini. Hali ni ngumu lakini ni muhimu kutumia fursa hii kusaidia zaidi suluhu inayoongozwa na Walibya.”

Mkutano huo mjini Tunisia umemjumuisha Federica Mogherini mwakilishi wa Muungano wa Ulaya kwa mambo ya nje na sera za usalama, Ahmad Abulgheit Katibu Mkuu wa Aran League, Moussa Faki , Mwenyekiti wa Tume ya Muungano wa Afrika na Ghassan Salame mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Libya.

Ghassan Salame kwa upand wake alisema, “Watu wa Libya, msipoteze fursa hii ya mapendekezo yaliyopitishwa wakati wa mkutano huu wa ngazi ya juu na msifunge dirisha hili la kujenga taifa lenye Umoja, la kiraia, lililo huru, lenye uwezo na usawa.”

Kwa muda mrefu tangu kuangushwa kwa utawala wa dikteta Muammar Gaddafi mwaka 2011 taifa hilo la Afrika  lililo katika bahari ya  Mediterranea limekuwa likigombewa na makundi yenye silaha ambayo yamesababisha kuporomoka kwa uchumi, miundombinu na usalama nchi nzima. Leo Libya imeanza uchaguzi wa majimbo katika manispaa tisa nchini humo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles