26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Rais wa Afrika kusini aicharukia ANC

Cape Town

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amekiri kuwa chama tawala nchini humo kilishindwa kudhibiti rushwa wakati wa utawala wa Jacob Zuma.

Ramaphosa amesema ANC haikuwapa raia wa Afrika Kusini kile ambacho walikuwa wanakitarajia kwa kuwajibika , wakati rushwa ilidhoofisha utawala wa sheria.

“Wote tunakubaliana kuwa taasisi ingeweza kufanya jitihada zaidi kuzuia utumiaji mbaya wa madaraka na matumizi mabaya ya rasilimali ,” alisema.

Rais ramaphosa amezungumza kama mkuu wa tume ya ANC na anatarajia kuendelea kutoa ushahidi wake siku ya Alhamisi.

Mwanzo wa maelezo yake siku ya Jumatano, alisema ANC ingejaribu kutoa mwanga wa namna jambo hili lingechunguzwa ili wahusika wawajibike.

Jacob Zuma anakabiliwa na mashtaka kadhaa ya rushwa ikiwemo ulaghai, mikataba ya uongo na utakatishaji fedha wakati akiwa madarakani kwa miaka tisa ingawa alikanusha kuhusika katika madai.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles