22 C
Dar es Salaam
Sunday, May 28, 2023

Contact us: [email protected]

Serikali yawaonya wenye maabara bubu

Na Derick Milton, Simiyu

Serikali imewataka wamiliki wa maabara binafsi zinazopima Magonjwa ya Binadamu, kuhakikisha wanafuata sheria na Kanuni katika kutimiza majukumu yao, ikiwemo kuajiri wataalamu sahihi wa maabara ambao wamedhibitishwa na serikali kupitia baraza lake la watalaamu wa maabara nchini.

Agizo hilo limetolewa leo Aprili 29, 2021 na Msajili Bodi ya maabara binafsi za Afya kutoka Wizara ya Afya, Dominic Fwiling’afu, wakati wa ufunguzi wa maazimisho ya wiki ya watalaamu wa maabara nchini kitaifa yanayofanyika katika Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu.

Fwiling’afu amesema kuwa wamebaini uwepo wa maabara bubu katika maeneo mbalimbali nchini ambapo kati ya Maabara 556 walizozikagua 68 zilikutwa hazifuati vigezo ikiwemo kufanya kazi bila ya kupata vibali na kuajiri wataalamu wasiostahili ambapo waliamua kuzifungia.

Dominic ameeleza kuwa ukaguzi huo ulifanyika Julai 2019 Hadi Mwezi Machi 2020 katika mikoa ya Dar es salaam, Mwanza, Kagera, Morogoro na Arusha, na kubaini watu wengi wanaanzisha maabara bila ya kufuata vigezo, hivyo akawataka kuacha mara moja tabia hiyo kwani kinyume cha sheria.

Amesema kuwa Bodi hiyo imeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha, ukaguzi wa mara kwa mara unafanyika kwa maabara zote binafsi zilizopo nchini, huku akawataka viongozi wa ngazi za chini kuanzia viongozi wa vijiji hadi halmashauri kutoka taarifa na ushirikiano katika kupambana na maabara bubu.

“Tumetoa mafunzo mbalimbali kwa viongozi wa halmashauri na watalaamu wake, katika kusaidia kukomesha maabara bubu, lengo la serikali siyo kunyima haki watu wawekeze katika sekta hii, lengo ni kuona wananchi wanatapatiwa huduma bora na zinatostahili.

” Niwatake wamiliki wote hawa wa maabara, kufuata sheria na taratibu katika uendeshaji wa shughuli zao, Kama bodi hatutasita kuchukua hatua kali kwa wale wote ambao tutawabaini wanaendesha shughuli za maabara kinyume cha utaratibu,” amesema Fwiling’afu.

Naye Msajili wa wataalumu wa Maabara kutoka Wizara ya a Afya, Mary Mtui amewataka watalaamu hao kuzingatia Maadili katika ufanyaji kazi wao, huku akiwataka waongozwe na maadilu ya taaluma yao na siyo kulazimishwa na wamiliki wa maabara ambao wengi wao wanatafuta pesa.

Amesema kuwa wapo wamiliki wa maabara wamekuwa wakiwalazimisha watalaamu wa maabara kutoa majibu ambayo siyo sahihi kwa wateja wao, lengo likiwa kupata pesa na siyo kutoa huduma iliyo bora kama ilivyo malengo ya serikali.

Almebainisha kuwa ofisi yake imeendelea kuwajengea uwezo watalaamu wa maabara nchini, huku ikichukuw hatua kwa wale wote ambao wamekuwa wakikiuka sheria na taratibu za Maadili ya taalimu yako ikiwemo kuwafutia usajili.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maazimisho hayo Rais wa Chama cha wataalamu wa Maabara nchini Yayha Mnung’a ameiomba serikali kuboresha kitengo cha mochwari katika hospitali mbalimbali na vituo vya Afya Kama ilivyo kwa vitengo vingine.

Mnung’a amesema kuwa kitengo cha mochwari kipo chini ya idara ya maabara, ambapo alisema kuwa kuna haja ya kitengo hicho kuboreshwa zaidi kwa kupatiwa vifaa Bora, majengo mazuri Kama ilivyo kwa idara nyingine katika sekta ya Afya kwenye vituo vya Afya, hospitali za rufaa za mikoa na Wilaya.

Naye Daudi Hemba Mtaalamu wa maabara kutoka Mkoani Pwani amesema kuwa chanzo cha uwepo wa maabara bubu nchini kinatokana na urasimu uliopo serikali hasa Wizara ya Afya pindi mtu anapohitaji usajili wa maabara yake kwani wengi wao ucheleweshwa.

“Kuna wakati mtu anazungushwa Sana, anatumia muda mwingi zaidi ya mwaka, anaangaika kupata usajili, wengi wakiona hivyo wanaamua kuendelea kufanya kazi bila ya usajili, lakini Kama Jambo hili litakomeshwa hakutakuwa na maabara bubu, ikiwezekana masula ua usajili yamalizikie huku Wilayani,” amesema Hemba.

Akifungua maazimisho hayo Kaimu Katibu tawala Wilaya ya Bariadi Isabela Nyaulingo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, amewataka watalaamu hao kuhakikisha wanazingatia sheria, Kanuni na taratibu zinazoongoza taalumu hiyo katika utenddaji kazi wao ili kuweza kuwa taifa lenye watu wenye Afya nzuri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,169FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles