32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 1, 2023

Contact us: [email protected]

Rais TFF kuburuzwa mahakamani

MalinziNA SAID MOHAMED, ZANZIBAR

ALIYEKUWA Makamu wa Rais wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Haji Ameir, amemjibu Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kwa kauli yake ya juzi ya kutoitambua kamati ya muda ya kusimamia soka la Zanzibar na anatarajia kumfikisha mahakamani ili kuthibitisha kauli hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View, Ameir alimshangaa Malinzi kwa kauli yake ya kutoitambua kamati  hiyo wakati alishaitambua kwa maandishi hapo kabla.

Juzi Malinzi alisema haitambui kamati ya ZFA na anamtambua rais halali wa ZFA, Ravia Idarous Faina.

Alisema kwamba, walifanya kikao na Rais wa TFF, Jamal Malinzi na kukubaliana kuwa kamati iliyopo ni sahihi na iendelee na shughuli zake.

“Jamal Malinzi anajua kila kinachoendelea katika mgogoro wa Zanzibar, tulifanya kikao alichokiitisha yeye mwenyewe na tulikubaliana kwamba kamati iliyoundwa ni sahihi kwa sababu ya hali halisi,” alisema Ameir.

Alisema ana nia ya kumpeleka Malinzi mahakamani ili kwenda kuthibitisha upotoshaji aliofanya kwa umma na anakamilisha taratibu yeye na jopo la mawakili wake ili wamburuze Malinzi mahakamani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles