32.2 C
Dar es Salaam
Thursday, February 2, 2023

Contact us: [email protected]

Kwanini Manchester United inaendelea kuwa na Van Gaal?

Louis-van-Gaal5MANCHESTER, England

KOCHA wa timu ya Manchester United, Louis Van Gaal, ameendelea kung’ang’ania kuwa katika timu hiyo, ingawa kiwango cha timu hiyo ni moja ya sababu ya kufukuzwa kwake.

Akiwa kwenye michuano ya Klabu Bingwa Ulaya msimu uliopita, alidai kwamba akili yake ilikuwa kwenye droo ya 16 bora na kujaribu kuelezea mbinu na mikakati  mbalimbali na matokeo yake aligonga mwamba.

Lakini ukweli ni kwamba Mdachi huyo hadi sasa yupo katika mgongo wa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ed Woodward, kwa kuwa makocha wachache wa aina yake  wasingeweza kudumu katika hali hiyo.

Hata hivyo, haifikiriwi kama bodi ya timu hiyo imeshindwa kufikiria kwamba hawana sababu ya kuamini kuwa maisha bila ya Van Gaal katika klabu hiyo yanawezekana na kuwa ya furaha zaidi.

Hadi sasa timu hiyo inatofautiana pointi tano na timu iliyoko nafasi ya nne ambayo inatarajia kucheza Klabu Bingwa Ulaya, huku ikiwa na tofauti ya pointi 10 na kinara wa ligi hiyo.

Matokeo hayo kwa namna yoyote yanaweza kuwa kikwazo kwa Van Gaal kuendelea kuwa kocha wa timu hiyo.

Manchester United katika miaka ya hivi karibuni imekuwa na hofu ya kufungwa na timu ndogo katika uwanja wa Old Trafford.

Klabu ya Southampton ilifanikiwa kupata ushindi Old Traffod, ingawa mchezo ulikuwa mgumu, hata kwa Norwich iliyofanikiwa kunyakua pointi tatu kwenye uwanja huo Desemba mwaka jana.

Pia klabu kama West Ham, Newcastle pamoja na Middlesbrough zilifanikiwa kupata sare katika uwanja huo msimu huu, huku Swansea, Southampton pamoja na West Brom zote zikifanikiwa kushinda msimu uliopita katika Uwanja wa Old Trafford.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles