26.1 C
Dar es Salaam
Friday, May 3, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia kufanyiwa maombi maalum

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Kanisa la Uamsho na Matengenezo ya Kiroho, limeandaa kongamano la maombi maalum ya kuliombea Taifa pamoja na  Rais Dk. Samia Suluhu Hassan yatakayofanyika Aprili 28,2024 kwenye viwanja vya Suma JKT, Mwenge jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa  habari leo Aprili 23,2024, jijini, Kiongozi wa kanisa hilo, Mwalimu Augustine  Tengwa amesema Mungu  ndiye aliyemsemesha juu ya maombi hayo kutokana na agano lake kwa Tanzania.

“Tangu mwezi wa kwanza aliponiambia Mungu, sikusema. Mungu amenisemasha mambo ambayo yatabeba ajenda ya siku hiyo ya maombi. Mungu kaniambia vitu vya kumuombea Rais,”ameeleza.

Amesema  sababu kubwa ya kuamua kuliombea Taifa na Rais Samia ni kutokana na kuwa kiulimwengu hakuna Taifa ambalo halifanana na Tanzania  hasa katika amani.

Mwalimu Tengwa amesema kuna mabadiliko ya kiuongozi ambayo Mungu anayaingilia kati, hivyo kuwataka watu wa dini zote kujitokeza katika maombi hayo.

“Nataka habari hii iende nchi nzima kuwa huu msimu wote ambao Mungu amenisemesha  kuanzia huu mwezi wa nne tutakuwa na maombi  mfurulizo ya  kumuombea Rais na Taifa  hadi muda wa uchaguzi ili kuondoa uovu,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles