23.8 C
Dar es Salaam
Sunday, May 12, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia kuanza ziara ya siku nne India kesho

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Rais Dk.Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya siku nne nchini India yenye lengo kudumisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili na kuendeleza ushirikiano katika sekta ya elimu, afya, maji na kilimo.

Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muumgano wa Tanzania kuelekea nchini India mwezi huu katika Ziara itakayo endeleza Ushirikiano na fursa mbalimbali.PICHA: IMANI NATHANIEL 

Rais Dk. Samia anatarajiwa kuondoka nchini Oktoba 8 kuanza ziara ya siku nne na atawasili nchini India na kupokelewa rasmi kwa ziara ya kitaifa na ataongozana na mawaziri wa wizara mbalimbali ili kuhakikisha sekta ya biashara na uwekezaji inakua nchini na kumaliza ziara Oktoba 11 mwaka huu.

Akizungumzia Oktoba 5, kuhusu ziara hiyo jijini Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amesema ziara hiyo inatarajiwa kuwa yenye tija kubwa kwa nchi kwani mikataba zaidi ya 15 itasainiwa.

“Ziara hii inafanyika kutokana na uhusiano mzuri uliopo baina ya India na Tanzania lakini pia kudumisha na kuendeleza uhusiano katika sekta za kimkakati ikiwemo elimu, maji, kilimo na afya,” amesema Makamba.

Amesema matarajio yanayotegemewa kutokana na ziara hiyo ni pamoja na kuanzisha taasisi ya upandikizaji moyo nchini lakini pia kuanzishwa kwa kiwanda cha chanjo za binadamu na mifugo.

Amesema pamoja na hayo wanatarajia mapinduzi ya kidigitali katika sekta viwanda kwa kuanzisha kiwanda cha kutengenezea simu janja nchini.

Akizungumzia kuhusu sekta ya kilimo Waziri Makamba amesema kwenye ziara hiyo inatarajiwa kuja na suluhisho la kudumu la soko la mbaazi nchini India kwani itatoa fursa kwa wakulima kulima zao hilo kibiashara kwani watakua na uhakika wa soko.

“Mbaazi ya Tanzania inaubora sana tutafanya mazungumzo na serikali ya India ili zao hili na mengine yawe na uhakika wa soko India na nchi nyingine,” amesema Makamba.

Aidha, amesema katika ziara hiyo mawaziri wa nchi zote watakutana na kuzungumza namna nzuri ya kushirikiana katika sekta mbalimbali ikiwemo uwanzishwaji wa kongani ya viwanda.

Amesema rais atapata nafasi ya kukutana na wafanyabiasha wakubwa 15 nchini huo ili kuzungumza nao kuja kuwekeza nchini katika sekta mbalimbali.

Sambamba na hayo, Serikali ya India itapata fursa ya kuja kuanzisha karakana ya vyombo vya usafiri wa majini hapa nchini.

Ameongeza kuwa wafanyabiashara 80 kutoka nchini wanatarajiwa kwenda kukutana na wafanyabiashara wa India lakini pia kituo cha uwekezaji TIC na ZIPA nao watashiriki ili kuonyesha fursa za uwekezaji zilizopo nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles