26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yahimiza Watanzania kulinda na kutunza raslimali za nchi

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Serikali imesema ni wajibu wa kila Mtanzania kulinda na kutunza raslimali za utalii kwa manufaa ya Taifa, vizazi vijavyo na ustawi wa utalii kwa ujumla.

Wito huo umetolewa Oktoba 6, na Waziri wa Maliasili na Utalii, Angela Kairuki wakati akifungua Maonyesho ya saba ya Kimataifa la Site Swahili Internation Tourism Expo yatakayofanyika kwa muda wa siku tatu yanashirikisha wadau mbalimbalikutoka ndani na nje ya nchi.

Amesema lengo la maonyesho hayo ni kuendelea na jitihada za kuongeza watalii nchini, ambapo jumla ya waoneshaji 150 na wanunuzi wa bidhaa 71 kutoka nchi tofauti wanashiriki.

“Viongozi wa mikoa endeleeni kuwa wabunifu katika maeneo yenu na kutangaza vituo vya utalii vilivyopo kwenye mikoa yenu na tunaendelea kukuza utalii maeneo mengine kwasababu tuna maeneo mengi ya utalii,”amesema Kairuki.

Amesema sekta ya utalii ni muhimu hivyo serikali na wadau wanawajibu wa kuendelea kutangaza vituo vyote vya utalii vya zamani na vipya nchini.

“Serikali inatambua umuhimu wa utalii hivyo kuendelea kuimarisha miundombinu, reli na viwanja vya ndege ili kuwawekea watalii mazingira bora na salama.

“Bado tunapenda kueleza kuwa hali ya watalii inakua kwa kasi ni kutekeleza lengo letu ifikapo mwaka 2025 kuwa na watalii milioni tano tunaendelea na juhudi za kuongeza watalii nchini,” amesema Kairuki.

Aidha, amesema wanaendelea kutoa ajira rasmi na zisizo rasmi na utalii makini kuleta watalii.

Naye Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Simai Mohammed Said amesema katika kuendeleza utalii lazima waboreshe miundombinu na kuondoa tozo ambazo ni kero kwa wananchi kusababisha kushindwa kufanya utalii wa ndani.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Damas Mfugale amesema S!TE Swahili International Tourism Expo wanatarajia kuwa onesho kubwa Barani Afrika na kuwavutia watalii mbalimbali duniani.

“Maonyesho haya yalianzishwa mwaka 2019 na hili ni onesho la saba hili la leo ni tofauti na miaka mingine tunaendelea kuongeza ubunifu na lengo letu ni kufanyika duniani onesho hili,”amesema Mfugale.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles