22.9 C
Dar es Salaam
Monday, September 9, 2024

Contact us: [email protected]

Bien Melody aingia rasmi kwenye gospo

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Baada ya kufanya muziki wa kizazi kipya kwa muda mrefu, mwanamuziki kutoka nchini Australia, Bien Melody, ameingia rasmi kwenye muziki wa Injili.

Akizungumza na www.mtanzania.co.tz Bien amesema tayari ameachia audio na video ya wimbo wake mpya wa Injili unaoitwa Only You huku akifuta nyimbo zake zote za kadunia kwenye mitandao.

“Nimeondoa nyimbo zote za Bongo Fleva kwenye mitandao, nimefungua chaneli mpya ya YouTube, Apple Music, Deezer na mitandao mingine ili nizidi kumtangaza Mungu na nimeachana kabisa na mambo ya dunia,” amesema Bien.

Aliongeza kuwa tayari wimbo wake Only You umetoka mwishoni mwa wiki na mashabiki wapya na wa zamani wanaweza kutazama video kwenye YouTube na kusikiliza kupitia Apple Music.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles