25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, May 4, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia aweka shada Mnara wa Uhuru wa Zambia na kaburi la Dk. Kaunda

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan leo Oktoba 24, 2023 ameungana na Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema, kuweka mashada ya maua kwenye Mnara wa Uhuru wa Zambia.

Rais Dk. Samia ameweka shada hilo ikiwa ni ishara ya kutoa heshima na kutambua walioongoza harakati za kuliltea uhuru Taifa hilo mwaka 1964.

Baada ya kuweka shada kwa mashujaa, Rais Samia pia ameweka shada la maua kwenye kaburi la Baba wa Taifa la Zambia, Dk. Kenneth Kaunda jijini Lusaka.

Leo Zambia inaadhimisha miaka 59 tangu ipate Uhuru kutoka kwa Waingereza mwaka 1964 na tukio la kuweka shada hufanywa kila mwaka wakati wa maadhimisho haya.

Rais Samia amealikwa kuwa mgeni rasmi kwenye tukio la maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru litakalofanyika baadaye leo kwenye Ikulu ya Zambia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles