25.5 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi 1,692 kufanya mtihani wa Darasa la Nne

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

JUMLA ya wanafunzi 1,692,802 wamesajiliwa kufanya upimaji wa kitaifa wa darasa la nne kesho, huku 759,573 wakiwa wa kidato cha pili wakitarajiwa kufanya Oktoba 30, hadi Novemba 09, mwaka huu.

Akizungumza leo Oktoba 24, jijini Dar es Salaam Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania(NECTA), Dk. Said Mohamed amesema kwa darasa la nne jumla ya shule za msingi 19,284 wanatarajia kufanya mtihani huo kuanzia Oktoba 25 hadi 26 mwaka huu.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dk.Said Mohamed

Amesema upimaji wa kitaifa kwa kidato cha pili utafanyika kwa jumla ya shule za sekondari 5,546 Tanzania Bara.

“Jumla ya wanafunzi 1,692 wamesajiliwa kufanya upimaji kitaifa wa darasa la nne, mwaka huu, kati yao wavulana ni 828,591 sawa na asilimia 48.95 na wasichana ni 864,211 sawa na asilimia 51.05,”amesema .

Amesema kati ya wanafunzi hao, 1,605,379 sawa na asilimia 94.84 watafanya upimaji huo Kwa lugha ya Kiswahili na wanafunzi 87,423 sawa na asilimia 5.16 watafanya Kwa lugha ya kiingereza ambayo wamekuwa wakitumia kujifunza.

Pia wanafunzi wenye mahitaji Maalum wapi 6,402 kati yao 1,074 ni wenye uoni hafifu, 93 ni wasioona, 1,240 wenye ulemavu wa kusikia, 2,209 mtindio wa ajili na 1,786 wenye ulemavu wa viungo vya mwili.

KIDATO CHA PILI

Dk. Mohamed ameeleza kuwa kati ya wanafunzi 759,573 waliosajiliwa kufanya upimaji wa kitaifa wa kidato cha pili mwaka huu, kati yao wavulana ni 353,807 sawa na asilimia 46.58 na wasichana ni 405,766 sawa na asilimia 53,42.

Amesema wanafunzi wenye mahitaji maalumu ni 1,382 kati yao683 ni wenye uoni hafifu, 82 ni wasioona, 290 ulemavu wa kusikia na 309 ulemavu wa viungo vya mwili na 18 ulemavu wa akili.

“Maandalizi ya upimaji kwa wanafunzi hayo yamekamilika ikiwa ni pamoja na kusambazwa Kwa karatasi za upimaji na nyaraka zote muhimu zinazohusu upimaji katika halmashauri zote nchini,” amesema.

Amesema upimaji huo kwa darasa la nne ni muhimu kwani unawezesha kujua kiwango cha wanafunzi katika kumudu stadi za juu za kusoma , kuandika na kuhesabu

Dk. Mohamed amesema umuhimu wa upimaji kidato cha pili, hupima uwezo na uelewa wa wanafunzi katika yote waliyojifunza Kwa kipindi cha miaka miwili ya masomo yao ya sekondari, upimaji wa kidato cha nne.

Aidha, ametoa wito kwa kamati za mitihani za mikoa na halmashauri zihakikishe kuwa usalama wa vituo vya mtihani unaimarishwa kwani vituo hivyo vinatumika kwa mujibu wa mwongozo uliotolewa na Baraza mtihani la Tanzania.

Vilevile aliwataka wasimamizi wote walioteuliwa kusimamia upimaji kufanya kazi yao ya usimamizi kwa umakini na uadilifu wa hali ya juu.

“Wasimamizi wanapaswa kuhakikisha kuwa, wanafanya kazi ya usimamizi kwa weledi na kwa kuzingatia kanuni za mitihani na miongozo waliyopewa ili kila mwanafunzi husika apate haki yake,” amesema.

Amesema wasimamizi hao wanapaswa kuhakikisha wanafunzi wenye mahitaji maalumu wanafanya upimaji wao ipasavyo ili wapate haki yao msingi ambazo ni pamoja na kupata mitihani yenye maandishi ya nukta nudu Kwa wanafunzi wasioona na maandishi yaliyokuzwa kwa wanafunzi wenye uoni hafifu.

Kwa upande wa wanafunzi amesema Baraza la mitihani halitarajii kuona mwanafunzi yoyote kujiusisha na vitendo vya udanganyifu na kutoa taadhari kuwa yoyote atakayebainika kufanya udanganyifu matokeo yake yatafutwa kwa mujibu wa kanuni za mitihani.

“Baraza linaamini kuwa walimu wamewaandaa vizuri katika kipindi chote cha miaka miwili ya elimu ya sekondari na miaka minne ya elimu ya msingi,” amesema.

Amewataka wamiliki wa shule kutambua kuwa shule zao ni vituo maalum vya mtihani na hivyo hawatakiwi kwa namna yoyote kuingilia majukumu ya wasimamizi wa mitihani katika kipindi chote cha ufanyikaji wa upimaji huo.

“Baraza halitosita kukifuta kituo chochote cha mitihani endapo linajiridhisha pasipo shaka kuwa uwepo wake unahatarisha usalama wa upimaji wa kitaifa,”amesisitiza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles