23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia ‘aupiga mwingi’ tena, IMF yaipa Tanzania trilioni 2.4

*Kusaidia kuimarisha uchumi ulioathiriwa na Uviko-19 na vita ya Urusi na Ukraine

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

RAIS Samia Suluhu Hassan ameupiga mwingi tena katika kuhakikisha kuwa uchumi wa Watanzania unaimarika na kuitoa Tanzania kwenye nchini maskini, hivyo ndivyo unavyoweza kusema.

Hii ni baada ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limeidhinisha mkopo wa dola za Marekani bilioni 1.046 ambayo ni zaidi ya Sh trilioni 2.4 kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kurejesha uchumi ulioathiriwa na janga la Uviko-19 na vita vya Urusi na Ukraine.

Fedha hizo unakuwa ni mkopo wa awamu ya pili kwa Tanzania kutoka IMF, ukitanguliwa na ule wa Septemba, mwaka jana, ambapo Tanzania ilipokea Sh trilioni 1.3 ulitolewa kwa ajili ya kukabili changamoto za kiuchumi zilizotokana na Uviko-19.

Makao Mkuu ya IMF.

Taarifa ya IMF iliyotolewa jana Jumanne Julai 19, imesema kuwa uchumi wa Tanzania unashindwa kuimarika kutokana na vita vya Urusi na Ukraine huku Uviko-19 ikiongeza changamoto.

“Uchumi wa Tanzania unashindwa kuimarika kutokana na vita hivyo, huku Uviko-19 ikizidisha changamoto katika maendeleo,” imeeleza taarifa hiyo.

Katika kipindi cha miezi michache iliyopita, Tanzania, kama ilivyo kwa nchi nyingine duniani, imeshuhudia kupanda kwa bei ya bidhaa mbalimbali, zikiwemo mafuta ya dizeli na petroli, ngano, mbolea na mafuta ya kupikia.

Hali hiyo imeilazimu Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, kuchukua hatua kadhaa za kupunguza gharama za maisha, kuendeleza miradi mikubwa na kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi nchini.

Sambamba na kutoa ruzuku ya Sh bilioni 100 kila mwezi kupunguza bei ya mafuta, hatua nyingine zilizochukuliwa ni kupaisha bajeti ya kilimo kutoka Sh bilioni 294 hadi Sh bilioni 954 ikiwa ni jitihada za kuinua uzalishaji wa ndani na kuchochea ajira.

Akiwasilisha bajeti ya Sh trilioni 41.48 kwa mwaka wa fedha 2022/23 bungeni jijini Dodoma mwezi uliopita, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, alisema Serikali itapunguza kiwango cha mafuta ghafi ya mawese kuanzia Julai 1, mwaka huu katika jitihada za makusudi za kupunguza mzigo wa mafuta.

Kabla ya hatua hiyo, mafuta ghafi yalitumika kuvutia ushuru wa asilimia 25 wa uagizaji ambao ulianzishwa mnamo 2018.

Rais Samia Suluhu Hassan.

Kutokana na hatua hizo, IMF ilionyesha kuunga mkono mpango wa uimarishaji uchumi wa Tanzania, huku wataalam wake wakisema kunahitajika msaada ili kufanya mageuzi ya kiuchumi.

Katika mkopo huo, Tanzania itapokea dola za Marekani milioni 151.7 ambazo ni zaidi ya Sh bilioni 349.

Mradi huo uliotangazwa na IMF ni sehemu ya Mpango wa Kuongeza Mikopo (ECF) unaolenga kusaidia kifedha na kuboresha utulivu wa kiuchumi kwa Tanzania, kufanya uwekezaji wa umma na kusaidia sekta binafsi.

“Kwa kutambua rekodi thabiti ya Tanzania katika utekelezaji wa mageuzi ya kiuchumi, wakurugenzi waliunga mkono maombi ya mamlaka ya kupanga utaratibu wa ECF ili kukidhi mahitaji ya dharura ya kifedha,” amesema Naibu Mkurugenzi Mkuu wa IMF na Kaimu Mwenyekiti wa bodi ya utendaji, Bo Li.

Hili ni jambo jingine la kupongezwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Samia Suluhu kwa kuendelea kuipigania Tanzania katika kila fursa Kimataifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles