25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, December 9, 2023

Contact us: [email protected]

DC Ileje aitaka TFS kutoa elimu kutunza misitu

*Akabidhi mifuko 20 ya saruji kwa vijiji 12

Na Denis Sikonde, Songwe

Mkuu wa Wilaya ya Ileje mkoani Songwe, Anna Gidarya ameitaka Wakala wa Misitu (TFS) wilayani humo kuendelea kutoa motisha na elimu kwa wananchi umuhimu wa uhifadhi wa misitu ili kuendelea kutunza misitu iliyopo ndani ya wilaya hiyo huku akikemea uwepo wa uvamizi.

Sehemu ya viongozi waliohudhuria kwenye hafla hiyo wakiwa katika picha ya pamoja.

Gidarya ameyasema hayo Julai 18, 2022 katika ofisi za hifadhi ya Iyondo Mswima zilizopo Katengele wakati akigawa vifaa vya ujenzi ikiwepo saruji, mipira na jezi vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 6 vilivyotolewa na wakala wa hifadhi ya misitu TFS wilayani humo kwenye baadhi ya vijiji na shule zinazoizunguka hifadhi hiyo.

Gidarya amesema TFS kutoa vifaa hivyo ikiwepo mifuko 20 kwa kila kijiji kwa vijiji 12 ni moja ya sehemu ya kuhamasisha jamii kulinda mazingira sambamba na kurithisha kizazi umuhifu wa mazingira huku akiwataka wenyeviti wa vijiji kwenda kutoa elimu kwa wananchi namna ya kutunza mazingira ili kulinda uoto wa asili uliopo.

Gidarya amesema utoaji vifaa hivyo ni motisha Kwa wananchi kutambua mchango wao namna wanavyoshiriki kuhifadhi msitu wa hifadhi ya Iyondo Mswima unaosimamiwa na TFS na kuwataka kushirikiana na viongozi wa wakala huo.

Gidarya ametumia nafasi hiyo kuwasihi madiwani kutumia mikutano ya hadhara kuhamasisha jamii kutokata miti ovyo, kutochoma moto kwenye hifadhi hiyo, kuchungia mifugo bali wawe mabalozi wa kutoa taarifa za watu watakaobainika wanajihusisha na shughuli za kibinadamu kwenye hifadhi ya Iyondo Mswima.

“Toeni elimu ili wajue ni marufuku kufanya shughuli zozote za kibinadamu ndani ya hifadhi ya msitu ambapo sio tu kulima hata kukata miti kwenye vyanzo vya maji kuwa ni kosa kubwa pia waelimishwe faida za utunzaji wa misitu.

“Ni marufuku kufanya shughuli zozote za kiuchumi katika msimu huu kuanza leo, eneo hili nila hifadhi kama kuna malalamiko yoyote yafuate taratibu na sheria na maelekezo ya serikali kwa mujibu wa sheria,” amesema Gidarya.

Vijiji vilivyokabidhiwa saruji ni Isoko, Sange Mswima, Itale, Ndapwa, Shikunga, Chilemba, Mbangala, Chikumbulu, Ngulugulu, Kalembo na Ngulilo.

Kwa upande wake, Mhifadhi mkuu wa shamba la miti Iyondo Mswima  Amiri Killo amesema kutokana na ushirikiano wa wananchi wameanza kutoa motisha kwa vijiji vinavyozunguka msitu wa hifadhi la Iyondo Mswima kwa kushiriki shughuli za maendeleo na michezo ili kuifanya jamii kutambua umuhimu wa  kutunza mazingira.

Killo amesema kwa kutambua mchango wa wananchi kwenye msitu huo wananchi hupewa Miche ya miti kwa ajili ya kupanda, kutoa saruji Kwa ajili ya maendeleo, jezi na mipira sambamba na ajira 450 kwa vijana.

“Wapo wanaovamia lakini tunaendelea kutoa elimu na kuhaamasiha kwa kuwashirika viongozi ili tuweza kuhifadhi japo zipo changamoto za uvamizi lakini tunajitajihidi kutoa elimu na matamko ili uhifadhi uweze kuendelea kwakuwa tunaaminini kuwa zipo faida nyingi endapo wananchi watalinda na kuhifadhi msitu hu.

“Shamba hilo lilianzishwa mwaka 2017 ambapo mpaka sasa zaidi ya hekta 954 zimepandwa miti zikisimamiwa na TFS, lina uwezo wa kuzalisha miche 500,000 Kwa mwaka hivyo kusaidia kufanya upanuzi wa upandaji miti kwenye hifadhi ya msitu wa Iyondo Mswima,”amesema Killo.

Akizungumza katika hafla hiyo diwani wa kata ya Kalembo wilayani humo, Leward Songa amesema watahakikisha jamii inapewa elimu ya kutosha juu ya umuhimu wa mazingira hususan baada ya kitambua mchango wa TFS kwenye shughuli za maendeleo kwenye vijiji vinavyozunguka hifadhi hiyo ili kulinda uoto wa asili.

Upande wake, Timotheo Mwamahonje ameishukuru TFS kwa kuwapa motisha ya vifaa vya ujenzi nakwamba kutasaidia jamii kuwa walinzi wa hifadhi hiyo na kuondokana na dhana ya awali ya kuweka uadui.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles