31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

RUWASA kutekeleza miradi 1,029 mwaka wa fedha 2022/23

Ramadhan Hassan,Dodoma

KATIKA mwaka wa fedha 2022/23, Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) umepanga kutekeleza jumla ya miradi 1,029 ambapo kati ya miradi hiyo 381 ni mipya na miradi 648 ni ile ambayo utekelezaji wake unaendelea kutoka mwaka wa fedha uliopita. 

Hayo yameelezwa leo Jumanne Julai 19,2022 jijini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA, Mhandisi Clementi Kivegalo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari

“Kiasi cha Sh 387,736,591,242 kimeishinishwa na Bunge kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo,”amesema.

Mkurugenzi Mkuu huyo amesema hadi kufikia mwishoni mwa mwaka wa fedha 2021/2022 jumla ya miradi 303 ilikuwa imekamilika na miradi 873 ilikuwa inaendelea na utekelezaji.

Amesema katika mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali kupitia Ruwasa ilipanga kutekeleza jumla ya miradi ya maji 1,527, ambapo kati ya hiyo, miradi 1,176 ilikuwa ni ujenzi wa skimu za usambazaji maji.

Amesema lisema miradi 351 ilikuwa ni ya utafutaji wa vyanzo vya maji chini ya ardhi na miradi 19 ilikuwa ni ya usanifu na jenzi wa mabwawa, ambayo baadaye hutumika kama vyanzo vya maji.

Mpango mkakati unalenga kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi waishio vijijini hadi kufikia kiwango kisichopungua asilimia 85 na hivyo kutimiza lengo la Ilani ya Chama Cha Mapinduzi(ccm) ya mwaka 2020 – 2025.

Wakati wa kuanzishwa kwake, RUWASA ilirithi jumla ya skimu za maji 1,379 zilizokuwa zimekamilika na kulikuwa na miradi 632 ya ujenzi wa skimu za usambazaji wa maji katika maeneo mbalimbali nchini. 

Kati ya skimu hizo zilizokamilika, 177 zilikuwa hazitoi huduma ya maji wa wananchi kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo changamoto ya kukauka kwa vyanzo vya maji. Wakati huo, yaani mwezi Julai 2019 upatikanaji wa huduma ya maji vijijini ulikuwa ni wastani wa asilimia 64.8. 

Amesema  utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2021/22, Serikali ilitoa fedha ya nyongeza ya    Sh bilioni 78.53 kupitia UVIKO– 19 kwa ajili ya kutekeleza miradi 172 ya maji vijijini.

Amesema  hadi kufikia mwezi Juni, 2022, jumla ya miradi 68 kati ya 172 imeanza kutoa huduma ya maji kwa wananchi na miradi iliyobaki inatarajiwa kukamilishwa mwishoni mwa Julai, 2022. 

“Kukamilika kwa miradi ya Uviko-19 kutawezesha jumla ya wananchi 1,036,071 kupata huduma ya maji safi na salama,”amesema Mkurugenzi huyo.

Mkurugenzi huyo amesema katika kuboresho huduma ya maji Msomera, Serikali kupitia RUWASA inaendelea na ujenzi wa bwawa la maji kwa gharama ya Sh bilioni 1.99 ambapo kwa sasa umefikia asilimia 15.

“Ujenzi wa bwawa hilo utakapokamilika, utasaidia kuboresha huduma ya maji kwa wananchi na mifugo yao pia.

“Kwa sasa, kati ya vijiji vyote nchini 12,319 ni vijiji 8,769 vinavyofikiwa na huduma ya uhakika ya maji safi na salama,” amesema Mhandisi

Amesema kwa mujibu wa tathmini iliyofanyika mwezi Aprili, 2022 upatikanaji wa huduma ya maji vijijini ulikuwa umefikia kiwango cha asilimia 74.5 ikiwa ni ongezeko la asilimia 9.7 ikilinganishwa na wastani wa 64.8 mwaka 2019. 

“Kasi hii, ni nzuri na tukienda kwa kasi hii, tunatarajia kuvuka lengo la asilimia 85 ifikapo mwaka 2025, kama ilivyoelekezwa na Ilani ya Chama cha Mapinduzi,”amesema Mkurugenzi huyo.

Amesema RUWASA inashirikiana na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na REA kubadilisha mifumo ya nishati ya uendeshati wa mitambo ya maji kutoka kwenye mfumo wa dizeli kwenda Mfumo wa Umeme jua (solar) na umeme wa TANESCO. 

“Hadi sasa, jumla ya skimu 19 kati ya 74 za mikoa miwili ya Singida na Dodoma tayari zimebadilishwa kwa kufungwa umemejua.  Kazi hii itaendelea kwa awamu kwa nchi nzima,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles