23.6 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Nicaragua amteua mkewe kuwa mgombea mwenza

Pics page Agosti 4RAIS Daniel Ortega wa Nicaragua amemteua  mkewe, Rosario Murillo kuwa mgombea mwenza wa urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika   Novemba mwaka huu.

Ortega (70), mwenye siasa za mrengo wa kushoto  anapewa  nafasi kubwa ya kushinda kwenye uchaguzi huo.

Alimtaja mkewe kama mgombea mwenza na makamu wa rais wakati  ambao anawania kuchaguliwa kwa   mara ya tatu.

“’Ni serikali ya umoja na Rosario Murillo ambayo ni kama ishara ya usawa wa jinsia,” alisema Rais Ortega.

Murillo tayari ni msemaji wa serikali na anaonekana kuwa anagawana mamlaka na mumewe.

Ortega aliwahi kutawala nchi hiyo miaka ya 1980 na baadaye akarudi katika madaraka mwaka wa 2007 kupitia chama chenye mrengo wa kushoto cha Sandinista National Liberation Front (FSLN).

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanawashutumu wanandoa hao  kwa kuiendesha Nicaragua   kama chombo chao cha  binafsi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles