27 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Rais wa Ufaransa ‘amtolea uvuvi’ Doland  rump

francoishollandePARIS: Ufaransa

RAIS   Francois Hollande wa Ufaransa amesema ushindi wa mgombea   urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican, Donald Trump katika uchaguzi ujao, unaweza kurejesha siasa  za zamani duniani kote na anawafanya watu ‘kujisikia kichefuchefu’.

Ushindi wa Trump   Novemba mwaka huu unaweza pia kuathiri uchaguzi wa  urais  Ufaransa utakaofanyakia 2017, alisema Hollande.

“Kama Wamarekani watamchagua Trump, watakuwa na wakati mngumu  kwa sababu uchaguzi wa Marekani ni uchaguzi wa dunia,” alisema alipozungumza na waandishi.

Taarifa ya Shirika la Habari la Uingereza, Reuters, inasema kiongozi huyo wa Ufaransa ametoa kauli hiyo baada matamshi ya Trump   kuhusu wazazi wa mwanajeshi Mmarekani muislamu aliyeuawa vitani nchini Irak.

Rais Barack Obama wa Marekani pia amemshambulia Trump hana sifa zinazostahili za  kuwa rais wa Marekani.

Naye  Trump alijibu mashambulio kwa kumshutumu Obama kama kiongozi aliyeshindwa na kwamba mgombea urais wa Democrat,  Hillary Clinton, naye hafai kuwania nafasi hiyo au  hata  ofisi yoyote   ya serikali.

Katika siku za karibuni, Tramp amekuwa akishambulia kila kona wakiwamo  wanachama wa chama chake cha Republican kama Richard Hanna  mwanachama mkongwe kutoka   New York ambaye alisema mgombea urais huyo  ni aibu kwa taifa.

Wanachama wengine wa Republican wamejitenga kumshabikia Trump au hata kutomuunga mkono.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles