24.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Museveni kuachia wimbo mpya

Yoweri_MuseveniKAMPALA, UGANDA

RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni, anatarajia kuachia wimbo wake mpya ambao ameupa jina la ‘Kwezi’ utakaokuwa unachangia shughuli za kampeni za uchaguzi.

Kwezi utakuwa ni wimbo wake wa tatu ndani ya miaka mitano mara baada ya kuachia wimbo wa Mpenkoni, ambao ulitumika sana katika kampeni za uchaguzi mwaka 2011.

Mpaka sasa rais huyo hajapanga siku ya kuuachia, lakini inasemekana ni siku za hivi karibuni kwa kuwa tayari amekaa na baadhi ya wataalamu wa muziki na kuupitia wimbo huo na wameupitisha.

Rais huyo anaamini kuwa wimbo huo mpya wa Kwezi utagusa idadi kubwa ya mashabiki na kufanya vizuri, huku akidai kuwa uchaguzi wa mwakani utakuwa na ushindani mkubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles