30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Filamu ya James Bond yazinduliwa Dar

spectreNa Theresia Gasper, Dar es Salaam

WADAU na watu maarufu mbalimbali hapa nchini mwishoni mwa wiki walijumuika katika uzinduzi wa filamu mpya ya Spectre James Bond iliyofanyika Cape Town Fish Market jijini Dar es Salaam.

Uzinduzi wa filamu hiyo iliyoigizwa na Daniel Craig kama James Bond, uliratibiwa na kampuni ya QWAY International chini ya udhamini wa kinywaji cha Belvedere Vodka ikishirikiana na Heineken, Jaguar pamoja na Land Rover.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla hiyo mwakilishi wa kampuni ya QWAY International, Tanya Mulamula, alisema hafla hiyo inalenga kuwakutanisha wadau na kuifurahia filamu hiyo mpya hasa kwa kuzingatia kuwa filamu ya James Bond ni maarufu sana duniani.

“Tunawashukuru Belvedere Vodca, Heineken, Landover na Jaguar ambao wameamua kwa pamoja kuwaunganisha wadau wa filamu hapa nchini kusherehekea uzinduzi wa filamu hii maarufu kwani baada ya hapa filamu hii sasa itaanza kuonyeshwa kwenye kumbi za sinema hapa nchini,” alisema.

Pia Mkurugenzi wa mauzo wa kampuni ya CMC inayohusika na magari ya Jaguar na Land Rover, Kim Withnall, alisema kuwa filamu hiyo imehusisha magari ya Jaguar na Land Rovers na ndiyo maana hata kwa Tanzania kampuni yake imeshiriki katika kuandaa hafla hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles