26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

Jeff Maximum akamilisha video ya Mama Afrika

jeff (1)Na Theresia Gasper, Dar es Salaam

MWANAMUZIKI wa R&B anayefanya kazi zake nchini Marekani na Dubai, Jeff Maximum, amekamilisha video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Mama Afrika ambayo aliitengenezea mjini Bagamoyo.

Video hiyo ambayo ilitoka rasmi mwanzoni mwa mwezi huu, tayari imeanza kuonekana kwenye vituo mbalimbali vya televisheini katika nchi mbalimbali za Afrika, Ulaya na Marekani. “Nilikuja kuitengeneza video hii hapa Tanzania lengo kubwa ikiwa ni kutangaza utalii wetu hapa nchini katika mataifa mengine kwa kuwa ninafanya kazi zangu nje niliona kuna haja ya kuja kufanya video ambayo itakuwa tofauti hivyo naionyesha dunia mandhari ya Tanzania ilivyo,” alisema Jeff.

Alisema video yake kwa sasa inafanya vizuri katika nchi za Dubai, Nigeria, Afrika Kusini, Kongo, Ghana na Uingereza na kwamba anafanya harakati za kuiachia nchini Marekani muda si mrefu na kwamba anaamini kupitia wimbo huo atakuwa ameiutangaza utalii wa Tanzania kwa kiasi kikubwa.

Video hiyo imetengenezwa na mwongozaji anayechipukia kutoka Tanzania, Hanscana (Wanene Films), huku audio yake ikiwa imetayarishwa katika studio ya One Vision Records iliyopo nchini Dubai.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles