33.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Papa Wemba, Weusi wafunga kazi Karibu Music Festival

Papa Wemba BagamoyoNa Mwandishi Wetu, Bagamoyo

MWANAMUZIKI nguli wa rhumba kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Jules Shungu Kikumba maarufu kama Papa Wemba na kundi la muziki wa hip hop la Weusi, juzi walifunga kazi kwa shoo zao kabambe kwenye tamasha la pili la Karibu Music Festival.

Tamasha hilo la siku tatu juzi lilishuhudia maonyesho makali kutoka kwa bendi mbalimbali zilizopanda jukwaani huku Papa Wemba na Weusi wao wakiwa wa mwisho kutumbuiza usiku huo.

Papa Wemba aliwapagawisha mashabiki kwa vibao vyake kadhaa maarufu kikiwemo kile cha Show me the Way ambacho ni kama kilikuwa kikisubiriwa kwa hamu na mashabiki waliohudhuria tamasha hilo.

Wengine waliofanya maonyesho na kuwa kivutio siku hiyo ni pamoja na Jhikoman, John Kitime na Inafrtica Band kutoka Tanzania. H art the Band kutoka Kenya iliyotamba na wimbo wake wa Uliza Kiatu pamoja na msanii Bo kutoka nchini Afrika Kusini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles