RAIS MUSEVENI ALIA NA MAUAJI

0
888

KAMPALA, Uganda


RAIS Yoweri Museveni, amesema kwamba amekasirika na kuumizwa na  vifo visivyo vya lazima kwa wananchi wake ambavyo vinajitokeza mara kwa mara nchini humu, lakini akasema kwamba ana uhakika hatua  za haraka zitachukuliwa ili kuwashughulikia wahalifu hao.

Rais Museveni alitoa kauli hiyo juzi wakati akiwahutubia maofisa usalama baada ya kukutana nao Ikulu ya nchi hii iliyopo mjini Entebbe.

Alisema wahalifu wamekuwa wakitumia mwanya wa asili ya upole walionao raia wa nchi hii na akawataka maofisa hao kuwa macho na watu hao.

“Wahalifu wanatumia faida ya upole walionao raia wa Uganda,” ila nawataka watu wote kuwa macho,” alisema Rais Museveni.

Katika mkutano huo ambao ni wa pili kulihutubia taifa ndani ya wiki moja, Rais Museveni, alisema kwamba mpaka sasa watuhumiwa 66 wameshatiwa mbaroni wakihusishwa na mauaji ya viongozi wa dini, watu wenye majina makubwa na hata watu wengine wa kawaida.

Hotoba hiyo ya Rais Museveni imekuja zikiwa ni siku chache, baada ya Kamanda wa zamani wa Polisi wa Wilaya ya Buyende, Muhammad Kirumira, kuuawa na watu waliokuwa wakitumia pikipiki, ikiwa ni baada ya kutokea mauaji mengine  ya Mbunge wa Jimbo la Arua,  Ibrahim Abiriga, Mkuu wa Polisi, Andrew Felix Kaweesi, Meja  Muhammad Kiggundu na Mwanasheria wa Serikali, Joan Kagezi.

Mbali na vigogo hao pia Mhasibu,  Susan Magara  na wanawake wengine katika miji ya  Entebbe, Nansana  na Masaka  na walipoteza maisha katika mauaji tofauti tofauti.

Akizungumzia vifo hivyo, Rais Museveni, alisema kwamba wengi wa wahusika wameshafikishwa mahakamani na kuhukumiwa huku wengine wakiwa wanaendelea kusakwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here