29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

WAZIRI SUDAN AKATAA WADHIFA

KHARTOUM, Sudan


WAZIRI Abdullah Hamduk, ambaye aliteuliwa juzi kushika wadhifa wa Waziri wa Fedha katika Serikali mpya ya nchi hii, anaripotiwa kukataa uteuzi huo.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la nchi hii, SUNA,  Hamduk ambaye ni Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa katika Idara inayoshughulikia masuala ya uchumi kwa Afrika, alikataa uteuzi huo juzi  na hivyo kumlazimu Rais  Omar al-Bashir kukabidhi jukumu hilo kwa Waziri wake Mkuu, Moataz Moussa Abdullah, kusimamia masuala hayo ya fedha.

Rais Bashir alitangaza bara hilo la mawaziri mapema wiki iliyopita na huku akisema kwamba ameamua kulipunguza ili kubana matumizi ya Serikali na kukabiliana na mfumuko wa bei na kupunguza pia uhaba wa fedha.

Kwa muda mrefu Serikali ya Khartoum imekuwa ikijaribu kupunguza  matumizi kama njia ya kukabiliana na mfumuko wa bei ambao umekuwa ukipanda kwa asilimia  64 kila mwaka  na Julai  mwaka huu ikajikuta inakumbwa na uhaba wa  fedha ambao umesababisha ugumu katika upatikanaji wa  mafuta na mkate.

Mwezi uliopita Chama tawala cha Rais Bashir kilisema kina mpango wa kuchagua utawala wa muda mrefu katika uchaguzi wa 2020 hatua ambayo itahitaji mabadiliko ya katiba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles