20.8 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Raila: Mpuuzeni Orengo kwa kutaka kumng’oa Ruto

Nairobi, Kenya

WAKATI harakati za kutaka kumng’oa Naibu Rais wa Kenya, William Ruto kwa tuhuma za ufi sadi zikishika kasi, Kiongozi wa Chama cha ODM, Raila Odinga, amesema hafurahishwi na mwandani wake, Seneta wa Siaya James Orengo kuongoza mpango huo.

Odinga anahisi harakati na matamshi ya Orengo yanaweza kuathiri uhusiano baina yake na Rais Uhuru Kenyatta na inasemekana amewaambia wabunge wa ODM kujitenga naye.

Odinga amekasirishwa zaidi na kauli ya Orengo kuwa, yeye na Rais Kenyatta wako katika mpango wa

siri wa kisiasa, kufuatia mwafaka wao wa Machi 9, 2018.

Siku moja tu baada ya Orengo kutoboa kuhusu mpango huo, Odinga alimtuma mwenyekiti

wa ODM John Mbadi kufafanua ukweli wa mambo.

“Nataka kufafanua kwa uwazi na uhakika kuwa, ODM haijaunda muungano wowote na chama ama mtu yeyote. “Maoni mengine yoyote ya kukinzana na haya yachukuliwe kuwa ya mtu binafsi,” Mbadi alisema katika majengo ya Bunge wiki mbili zilizopita.

Inasemekana Rais Kenyatta pia hakufurahishwa na matamshi ya seneta huyo, hasa aliposema kuwa alikutana naye kwa saa nne.

Matamshi hayo yalipandisha joto katika kambi ya Naibu Rais, ambapo wafuasi wake wanahisi ni Rais anajaribu kumhujumu Dk Ruto, kinyume na makubaliano yao kuwa angemuunga mkono baada ya kukamilisha muhula huu wake mwaka 2020.

Ujumbe wa Orengo umetoa fursa kwa Dk. Ruto na kambi yake kuendelea kukosoa mwafaka baina ya Rais Kenyatta na Odinga, wakisema ulilenga kumzuia Ruto kuingia Ikulu.

Mzozo huu ulianza mwaka jana kabla ya Rais Kenyatta kuzuru Nyanza wakati Orengo alipowaongoza viongozi wa eneo hilo kudai watu walioathiriwa wakati wa uchaguzi uliopita wafi diwe.

Odinga hakufurahishwa na wito huo, akisema haukuwa muda mwafaka wa kujadili mambo hayo.

“Uhuru amekubali kufanya kazi nasi na mambo mengine kama haya yanaweza kusuluhishwa ndani si kwa mikutano ya hadhara.

Huu si wakati wa uanaharakati, tumejaribu hiyo njia na haikufanya kazi, kwanini tusijaribu mbinu nyingine,” Raila alikaririwa akiwaeleza viongozi wa eneo hilo wakati wa ziara ya Kenyatta.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari ndani ya ODM, Odinga alimtaka Orengo kumweleza sababu ya kusukuma ajenda ya kumng’oa Naibu Rais na faida atakayopata.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,058FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles