23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

PROFESA NDALICHAKO AWAPA MAAGIZO MAOFISA ELIMU

Na JANETH MUSHI -ARUSHA


WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, amewataka maofisa elimu wa shule za msingi na sekondari nchini, kuhakikisha vyama vya skauti vinakuwa na masomo ya ziada katika shule hizo.

Aidha, ametoa wito kwa viongozi wa skauti barani Afrika, kuimarisha skauti kwenye nchi zao na kuhakikisha wanaungana, ikiwa ni pamoja na kupiga vita unyanyasaji dhidi ya akinamama na watoto.

Profesa Ndalichako ambaye pia ni Rais wa Chama cha Skauti Tanzania, aliyasema hayo juzi jijini hapa kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, katika maadhimisho ya siku ya skauti Afrika ambayo kwa mwaka huu yalifanyika nchini.

Alisema katika maadhimisho hayo, vijana kutoka shule mbalimbali hapa nchini walipaswa kuwa wengi kwani kupitia mafunzo hayo wanajifunza uzalendo, ukakamavu na kuwa na moyo wa kujitolea kwa ajili ya Taifa lao.

"Kama rais wa skauti na waziri mwenye dhamana ya elimu, naomba nitoe wito kwa maofisa elimu wote wa mikoa kuhakikisha suala la skauti shuleni linakuwa ni sehemu ya masomo ya ziada.

“Nasema hivyo kwa sababu mikoa mingine hapa washiriki ni wachache na nauliza kwanini tunawanyima vijana kushiriki kwenye mambo ambayo yana manufaa kwa Taifa.

"Tunataka wafanye nini, wakienda vijiweni hatuwaruhusu, hivyo tuwatengenezee mazingira na tutumie nguvu walizonazo katika mambo yatakayowajenga kuwa raia wema.

“Wakijiunga na skauti itawaongezea moyo wa kujitolea na kulipenda Taifa lao kwani kuna  baadhi ya mikoa maofisa elimu hamjafanya kazi kikamilifu ndiyo maana klabu hazina nguvu.

“Kwa hiyo, nawaomba mkaziimarishe klabu hizo ili ziwe na nguvu zaidi kwa sababu zina umuhimu kwa vijana wetu,” alisema Profesa Ndalichako.

Awali, Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania, Mwantumu Mahiza, alisema wanakusudia kupeleka skauti katika vyuo vikuu ili kusaidia jamii kuhuisha maadili ya vijana ambayo kwa sasa yameanza kushuka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles