27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

PROFESA MUHONGO AZINDUA MAFUNZO TAA, CHAJA ZA MWANGA WA JUA

Na MWANDISHI WETU-MARA


WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amezindua mafunzo ya namna ya kutengeneneza taa na chaja zinazotumia mwanga wa jua kwa vijana 20 wa Kata ya Nyegina, Mkoa wa Mara.

Akifungua mafunzo hayo juzi, Profesa Muhongo aliwataka vijana hao kuwa mabalozi wazuri wakati wanapohudhuria mafunzo na kueleza kuwa yatakuwa chachu katika kupanua wigo wa ajira ikiwemo wahitimu kujiajiri wenyewe.

Aliwataka vijana na wananchi mkoani humo kuweka nguvu kubwa katika elimu kutokana na umuhimu na mchango wake kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Kuhusu Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini Awamu ya Tatu, Profesa Muhongo, alieleza kuwa itaanza kutekelezwa kuanzia Machi na kusisitisza kuwa, azma ya Serikali ni kuhakikisha kuwa katika kipindi cha miaka mitano vijiji vyote nchini viwe vimeunganishwa na nishati hiyo.

"Vijiji vyote vitaunganishwa na nishati ya umeme. Tutasambaza awamu kwa awamu na lengo letu ni kuhakikisha kuwa vijiji vyote chini vinaunganishwa na umeme ndani ya kipindi cha miaka mitano. Wale ambao hawajafikiwa awamu ya kwanza na ya pili tutawafikia awamu ya tatu vivyo hivyo mpaka tufikie lengo letu,” alisisitiza waziri huyo.

Kwa upande wake Balozi wa Korea Kusini nchini, Song Geumyoung ambaye nchi yake imefadhili mafunzo hayo, alisema uwepo wa taa hizo utasaidia upungufu wa umeme hususan maeneo ya vijijini na ambayo bado hayajaunganishwa na nishati hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles