23.2 C
Dar es Salaam
Monday, February 6, 2023

Contact us: [email protected]

TRA YAWANOA WATAALAMU WA KODI

NA ASHURA KAZINJA-MOROGORO


MAMLAKA ya Mapato Tanzania  (TRA) imetoa mafunzo kwa wataalamu  wa elimu kwa mlipa kodi mkoani Morogoro,  juu ya Sheria Mpya ya mwaka 2014 katika sheria ya kodi ya ongezeko la thamani  (VAT), usimamizi wa kodi na kodi ya zuio (withholding tax).

 Akizungumza katika mafunzo hayo juzi, Meneja wa elimu kwa mlipa kodi, Diana Masala, alisema mafunzo hayo yana lengo la kuwajengea uelewa wa sheria hiyo mpya ya kodi la ongezeko la thamani VAT, usimamizi wa kodi na  kodi ya zuio ili wawe wawakilishi wazuri wa sheria hiyo kwa jamii.

Masala alisema sheria hiyo mpya haimruhusu mfanyakazi wa TRA  kwenda ofisini kwa mteja peke yake na kwamba wote watapewa vitambulisho ambavyo vitakuwa na namba ya simu ya TRA na asiyekuwa nacho, mteja asikubali kuzungumza naye ili kuepuka utapeli.

 

Akizungumzia ubadilishaji wa TIN,  Masala alisema ni kwa ajili ya kupata taarifa sahihi, idadi, aina ya wafanyabiashara, wako wapi  ili kuisaidia Serikali katika kupanga mikakati yake ya kiuchumi.

 

 “Mfano TIN ambayo si ya biashara ni ile unayoomba kwa ajili ya kukusaidia  kutoa gari lako bandarini uliloliagiza kutoka nje, pia unaweza kubadili TIN yako isiyo ya biashara kuwa ya biashara ukitaka,” alisema Masala.

“Sheria hii ya mwaka 2014 inasema msamaha una jedwali moja tu ambalo lina sehemu moja na  mbili  tofauti na sheria ya zamani iliyokuwa na sehemu tatu ambayo ilikuwa na unafuu wa kodi, iliyosamehewa kodi na inayotozwa kodi kwa asilimia sifuri, hivyo chochote  ambacho hakipo katika jedwali la msamaha kitatozwa kodi,” alisema.

Awali Meneja wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi, Gabriel Mwangosi, alisema vitu vilivyosamehewa kodi ni vile muhimu zaidi kwa maisha ya jamii kama kilimo, afya, elimu, walemavu, uvuvi na vingine, huku dini ikiwa haimo huku akisisitiza kuwa atakayenunua bidhaa bila kupewa risiti na hakutoa taarifa anakabiliwa na faini ya Sh 30,000.

Baadhi ya washiriki wa semina hiyo, Rehema Mmari na  Samsoni Mniwe waliiomba TRA kubainisha kamisheni za mawakala wa tigo pesa ambao wanakatwa asilimia 10 lakini hawazipati.

Changamoto nyingine iliyoainishwa ni mashine nyingi za kutolea risiti kuharibika mara kwa mara na bei ya mafundi kutoeleweka kwani baadhi yao hutoza gharama kubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles