30.8 C
Dar es Salaam
Saturday, January 28, 2023

Contact us: [email protected]

WADAU WAOMBWA KUSHIRIKI HARAMBEE YA KILIMO BIASHARA

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


TAASISI isiyo ya kiserikali ya Land O’ Lakes, imewaomba wadau wa kilimo na biashara nchini kushiriki kwenye harambee inayolenga kukusanya Sh milioni 150 kwa ajili ya kuwezesha mradi wa kuwajengea uwezo wanawake kushiriki katika kilimo biashara Alhamisi wiki hii. 

Harambee hiyo itaongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, jijini Dar es Salaam, huku kiasi cha fedha kitakachopatikana kikitarajiwa kuelekezwa katika kuijengea uwezo wa kiutendaji taasisi inayojihusisha na kuendeleza wanawake katika kilimo Tanzania (CAWAT).

Harambee hiyo imebeba kauli mbiu ya ‘Wezesha kilimo biashara kwa ajili ya ajira, jamii na viwanda endelevu’.

“Mafanikio tutakayoyapata kupitia harambee hii yataiwezesha CAWAT kutoa mafunzo na kuwajengea uwezo wanawake wanaojishughulisha na kilimo hapa nchini kubadilika na kujikita zaidi katika kilimo biashara kwa maana kwamba watajengewa uwezo wa kufahamu fursa za masoko ya bidhaa wanazozalisha, kujitangaza pamoja kuwaunganisha na wawekezaji wakubwa,” alisema Mkurugenzi wa Mradi kutoka Land O’ Lakes, Dk Rose Kingamkono.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles